Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kulia)
akimkabidhi Bendera ya Taifa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi
Rajabu ambaye ndiye kiongozi wa Timu ya Mabalozi wa Tanzania walioanza
zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza mlima na
kuvutia wageni wengi zaidi nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa akitoa maelezo ya Mlima Kilimanjaro kwa Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe
akizungumza na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi muda mfupi
kabla ya kuzindua safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la
kuutangaza ili kuvutia watalii wengi nchini.
Baadhi
ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakisikiliza kwa
makini hotuba zilizokuwa zikitolewa kabla ya uzinduzi rasmi wa zoezi lao
la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza ili uweze kuvutia
wageni wengi zaidi nchini.
Mabalozi
wakiwa tayari kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika lango
la Marangu. Kutoka kushoto ni Dk. Batilda Burian; Daniel Njoolay; Aziz
Mlima; Joseph Sokoine na Ramadhani Mwinyi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru akitoa neno la
ukaribisho kwa Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe na kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa.Balozi
wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajab pamoja na timu ya mabalozi
anayoiongoza kupanda Mlima Kilimanjaro akinyanyua juu bendera ya taifa
pamoja na kushangilia ikiwa ni ishara ya kuuthamini Mlima Kilimanjaro
ambo ni chachu muhimu ya utalii nchini.
……………………………………………………………………………..
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe
amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali
ulimwenguni kuhakikisha kuwa wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo
nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza diplomasia ya uchumi.
Waziri
Membe aliyasema hayo wakati akizindua zoezi la kupanda Mlima
Kilimanjaro linalofanywa na mabalozi mbalimbali wanaoiwakilisha Tanzania
nje ya nchi kwa lengo la kuutangaza Mlima Kilimanjaro ili uweze kuvutia
watalii wengi zaidi.
“Bado
idadi ya watalii wanaofika nchini kupanda mlima hairidhishi na jitihada
kubwa zinahitajika kufanywa na mabalozi kuhakikisha kuwa wanautangaza
vema mlima kwa kuwa ni hazina ya pekee tuliyonayo inayopaswa kuwa kitega
uchumi kizuri kwa uchumi wan chi yetu” alisema Membe.
Jumla
ya mabalozi 14 wanashiriki zoezi hili ambalo litakuwa likifanyika kila
mwaka kwa lengo la kuutangaza Mlima Kilimanjaro. Mabalozi hao ni pamoja
na Adadi Rajabu (Zimbabwe); Ramadhani Mwinyi (Umoja wa Mataifa); John
Kijazi (India); Batilda Burian (Kenya); Shamim Nyanduga (Msumbiji);
Grace Mujuma (Zambia); na Patrick Tsere (Malawi)
Wengine ni pamoja na Mbarouk Mbarouk (Saudi Arabia); Joseph Sokoine (Mkurugenzi Bara la Amerika); Ladislaus Komba (Uganda); Azizi Mlima (Malaysia); Radhia Msuya (Afrika Kusini); Daniel Ole Njoolay (Nigeria) na Charles Sanga (Balozi mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii )
Wengine ni pamoja na Mbarouk Mbarouk (Saudi Arabia); Joseph Sokoine (Mkurugenzi Bara la Amerika); Ladislaus Komba (Uganda); Azizi Mlima (Malaysia); Radhia Msuya (Afrika Kusini); Daniel Ole Njoolay (Nigeria) na Charles Sanga (Balozi mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii )
No comments:
Post a Comment