Wanamgambo wa al-shabaab wanaaminika kutekeleza mauaji hayo.
Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa
kundi la Al Shabaab wamewauwa kwa kuwapiga risasi zaidi ya watu 28
waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja karibu na mpaka wa Somalia.
Maafisa wa ngazi ya juu wamesema kuwa basi hilo lilitekwanyara katika
Jimbo la Mandera wakati likiwa njiani kuelekea katika mji mkuu Nairobi.
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limetekeleza mashambulizi kadhaa
nchini Kenya tangu mwaka 2011.Huo ndio mwaka ambapo Kenya iliwatuma
wanajeshi wake nchini Somalia kupigana na kundi hilo la waislamu wenye
itikadi kali.Mji wa Mandera katika eneo la Kaskazini mashariki ndio
ulioathirika pakubwa. Baada ya shambulio hilo la mapema jumamosi maafisa
katika eneo hilo wamenukuliwa na vyombo vya habari nchini kenya
wakisema kuwa serikali ilikataa kuitikia ombi lao la kutaka usalama
kudumishwa zaidi.Afisa mmoja ameliambia gazeti la Daily Nation kwamba
wavamizi hao waliwataka abiria kusoma aya katika Koran kabla ya
kuwaangamiza walioshindwa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment