Wazazi wa
Miss Tanzania mpya, Lilian Kamazima wameitaka Kamati ya Miss Tanzania
iwape maelezo ya uhakika kuhusu zawadi na taji la binti yao kwa kuwa
hadi sasa wako njiapanda. Kauli hiyo ya Eva na Deus Kamazima imekuja
siku chache baada ya mrembo huyo kuwasili jijini Arusha akitokea Dar es
Salaam.
Wakizungumza
nyumbani kwao, Majengo Juu jijini Arusha jana, wazazi hao walionyeshwa
kushangazwa na hatua ya kumpokea binti yao akiwa hana taji, pamoja na
fedha ambazo alistahili kupatiwa kama mshindi.
Walisema
kuwa walimpokea binti yao kama ‘yatima’, hata tiketi ya ndege
alilazimika kulipiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Investment Ltd, aliyemuibua katika ngazi ya Kanda ya Kaskazini.
“Tunaiomba Kamati ya Miss Tanzania itupe maelezo ya kina kuhusu zawadi, taji pamoja na vitu vingine kwa kuwa tumempokea binti yetu kama bila zawadi wala taji,” walieleza wazazi hao kwa nyakati tofauti. Awali, mrembo huyo alisema kuwa pamoja na kwamba bado hajakabidhiwa taji wala zawadi yoyote na Kamati ya Miss Tanzania, lakini kitendo cha kupewa kiti hicho ameridhika
No comments:
Post a Comment