Mwakilishi
wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India
(SEWA), Labhu Thakkar akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Kuranga wakati walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo
wilayani hapo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila na mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akizungumza na Wanachama
wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA)
walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga
Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini
Kidete. Kushoto ni mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia
ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi
wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India
(SEWA), Labhu Thakkar walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo
Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya
kijiji cha Msufini Kidete.
Mkutano
ukiendelea kabla ya wageni kutoka Ushirika wa Wanawake waliojiairi
wenyewe kutoka India (SEWA) kutembelea Zahanati ya Kijiji cha Msufini
Kidete iliyopo Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Wachama wa Ushirika Sewa wakiwa katika mkutano na uongozi wa Kijiji cha Msufini Kidete Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Mtendaji
wa Kijiji cha Msufini Kidete, Seleman Kayombo akitoa taarifa fupi za
utendaji wa kijiji hicho kwa wageni waliofika kutoka Ushirika wa
Wanawake waliojiajiri wenyewe kutoka India (SEWA) walipotembelea
Zahanati ya Kijiji hicho.
Mkurugenzi
wa Mradi wa Sankalit Sewa, Shree Kant Kumar akizungumza wanakijiji wa
Msufini Kidete wakati Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka
India (SEWA) walipotembelea miradi ya maendeleo ikiwemo afya.
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Msufini Kidete wakiwasikiliza wageni
waliofika kijijini hapo kutoka katika Ushirika wa Wanawake waliojiairi
wenyewe kutoka India (SEWA), walipotembelea Zahanati ya kijiji cha
Msufini Kidete Mkuranga.
Zahanati ya Kijiji cha Msufini Kidete.
Huduma za afya zikiendelea katika Zahanati ya kijiji.
Baadhi ya wagonjwa wakisubiri huduma za matibabu katika Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete Mkuranga.
No comments:
Post a Comment