Waziri
wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi aongoza zoezi la kupima afya za Wabunge
katika Ukumbi wa Msekwa jana.Upimaji wa afya za Wabunge umefanywa na
Madaktari wa Aga Khan kutoka Morogoro,Dar. na Dodoma.
Waziri
wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi (kulia) akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa
Hospitali ya Agha Khan,Sisawo Konteh wakati wa zoezi la upimaji wa Afya
kwa Waheshimiwa Wabunge,Mjini Dodoma jana.Katikani ni Mmoja wa Maafisa
waandamizi wa Hospitali ya Agha Khan.
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Vijijini,Mchungaji Luckson Mwanjale akimsikiliza kwa
Makini Mtaalam wa Maswala ya Afya kutoka Hospitali ya Agha Khan wakati
wa zoezi la kupima Afya kwa waheshimiwa Wabunge,Mjini Dodoma jana.
Mh. Zakhia Meghji akipewa maelezo na Daktari Raheel Kanji wa Hospitali ya Agha Khan
Mh. Mbunge akifanyiwa vipimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya akijiandaa kupima uzito wake.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi
Juma akipima akichukuliwa vipimo na Daktari kutoka Hospitali ya Agha
Khan.
Ushauri.
Waziri wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi akiongea na wanahabari juu ya zoezi la upimaji Afya kwa Waheshimiwa Wabunge aliloliongoza.
Waheshimiwa Wabunge wakiendelea kumiminika kwenye Ukumbi wa Msekwa,Bungeni Mjini Dodoma ili kushiriki zoezi la upimaji Afya.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini zoezi hilo.Picha zote na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii,Kanda ya Kati.
No comments:
Post a Comment