Wakati Barack Obama akiingia katika mji kwa ajili ya mkutano wa G20 nchini Australia, inaonekana alikuwepo mtu mwenye sura kama yake ambaye hakuwa mbali nae.
Wakati Rais alikuwa anaendeshwa katika mitaa ya Brisbane gari lake aina ya limousine lilikuwa linalindwa vilivyo,"Mnyama" Barack Obama alipigwa picha na waandishi wa nchini humo na kuonekama kama sio yeye.
Mtu ambaye hakutajwa akifanana kabisa na Obama hata kutimiza wajibu wa kuwapungia mkono umati wa watu uliokuwa ukimngoja, gazeti la Courier-Mail limeripoti .
Kama hii ilikuwa ni mtu aliye na mwonekano wa rais, siyo mara ya kwanza kiongozi wa ulimwengu kuwa na watu wenye sura au mwonekano unaofanana na wao kwasababu za usalama wao.
Ikumbukwe Dikteta wa zamani Saddam Hussein inaonekana alikuwa na watu waliokua na sura kama yake wakati wa muda wake akiwa mkuu wa Iraq na pia imedaiwa kuwa kiongozi wa Nazi Adolf Hitler alikuwa na watu hadi sita.
No comments:
Post a Comment