Raia wengi kutoka Ulaya wamejiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria
Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi amewasili
nchini Uturuki baada ya safari iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya
kumchukua binti yake aliyekua mjini Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa
Islamic State.Monique alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti
yake aitwae Aicha kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa
kundi hilo mwenye asili ya Uholanzi na Uturuki.Mamia ya Wanamgambo
wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la
IS.Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na
IS.Raia wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria
Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa.Aicha aliondoka Uholanzi
mwezi Februari, akaolewa na Omar Yilmaz, mwanamgambo mwenye asili ya
Uturuki na Uholanzi ambaye alishawahi kuwa mwanajeshi nchini
Uholanzi,alitumia mbinu alizopatiwa akiwa mwanajeshi na kuwafunza
wapiganaji wenzake.
Monique amesema mwanae alibadilika ghafla kutoka binti aliyefahamika vyema na kuwa Msichana mwenye msimamo mkali.
Baada ya Polisi kumuonya Aicha
kutosafiri kwenda Syria walikamata Pasi yake ya kusafiria, Aicha
hakuvunjika moyo alitumia kitambulisho chake.
Aicha alikuwa akiwasiliana na Yilmaz kwa njia ya mtandao wa kijamii kisha wakapendana.
Monique alisafiri mpaka Uturuki mwezi Oktoba ili kumchukua mtoto wake lakini alishindwa kuvuka mpaka.
Lakini wiki iliyopita, baada ya Aicha
kuomba msaada alirudi tena nchini Syria ingawa Polisi walimkataza
kufanya hivyo.Monique alifika Raqqa nchini humo na kumchukua bintiye
kisha kurejea Uturuki
Yilmaz, Mume wa Aicha anamtaja mkewe kuwa mtalaka wake kwenye anuani yake ya Tweeter.
Hivi sasa Mama na mwana wanashikiliwa mpakani mwa Uturuki, wakisubiri ruhusa ya kurudi Uholanzi.
Serikali ya Uholanzi imeiambia BBC
kuwa inawasiliana na Monique lakini haijatoa ufafanuzi zaidi, tatizo ni
kuwa Aicha hana Pasi ya kusafiria ingawa mwanasheria wake anasema huenda
wakarejea Uholanzi ndani ya wiki moja.-BBC
No comments:
Post a Comment