Tumekua
tukizipata taarifa za watu mbalimbali kukamatwa na dawa za kulevya
kwenye viwanja vya ndege pamoja na sehemu nyingine za kusafirishia
ambapo kila mmoja amekua na mbinu yake kusafirisha mzigo huo
haramu.Stori mpya ya leo imetokea Nigeria ambapo mwanaume aitwae Mama
Solomon kutoka Enugu amekamatwa kwenye uwanja wa ndege Lagos akiwa
ameficha dawa za kulevya aina ya Cocaine katikati ya soli ya kiatu cha
Mwanamke.
Jamaa
alikua akitokea Brazil ambayo ni nchi maarufu sana kwa kuziuzia nchi
nyingine dawa za kulevya na alikua na mifuko miwili iliyojaa viatu vya
Wanawake na pochi.
Baada ya
kukamatwa, Solomon mwenye umri wa miaka 27 alikataa dawa hizo kuwa za
kwake na kusema yeye amekua akifanya kazi na kuishi nchini Brazil hivyo
kuna rafiki yake alimpatia huo mzigo na kumwambia akiufikisha salama
atazawadiwa.
No comments:
Post a Comment