Habari
zilizotufikia kutoka Mwanga Mkoani Kilimanjaro zinasema kuna ajali mbaya
imetokea maeneo ya Mwanga wakati basi la kampuni ya Mbazi Travellers
lililokua likitokea Arusha kuelekea Dar es salaam kupinduka.
Taarifa
zinasema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kujaribu kulipita basi
jingine huku kukiwa hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini inasemekana
kuna idadi kubwa ya majeruhi ambao walikimbizwa katika hospitali ya KCMC
Moshi.
No comments:
Post a Comment