Pages

May 18, 2014

WATU WATANO WAFARIKI MCHANA HUU 16 WAJERUHIWA SINGIDA

Leonard Manga,Singida
WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo la abiria aina ya "hiace" eneo la Mlima Sekenke, wilayani Iramba kwenye barabara kuu ya Singida - Mwanza.

Mganga wa zamu katika hospitali ya Wilaya ya Iramba, Dk Antony Mbulu alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi Mei 17 majira ya saa 2:30 usiku ambapo iliwahusisha abiria hao ambao walikuwa wanaenda kwenye sherehe ya Maulid kijiji jirani cha Shelui na kwamba walipokea miili ya watu watano na majeruhi 16.

Dk Mbulu aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo ni pamoja na dereva Athuman Adam (34), Ally Ibrahimnu Wambura (36) wakazi wa Igunga na Amin Seif Salim (45) mkazi wa mjini Singida wakati miili ya watu wawili haikuweza kutambuliwa.

Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dreva wa basi hilo lenye namba za usajili T547 ASP kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi

Alisema kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo wamehamishiwa hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi huku hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya.

Kwa mujibu wa Mganga huyo wa zamu ajali hiyo ilitokana na ni mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani ambapo dereva huyo alidaiwa alikuwa akiyapita malori kwa kasi hali iliyosababisha gari kugonga kingo za barabara na kupasuka tairi.kabla ya kuingia msituni na kupinduka mara nne.

Alisema kuwa basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 na kwamba lilikuwa likitokea mjini Singida kwenda Shelui.
Like · ·

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...