Pages

May 13, 2014

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ZAKABILIWA NA URASIMU WA AJIRA NA BIASHARA

Katibu Mkuu wa EAC,Dk Richard Sezibera

Mwandishi wetu Arusha
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera amesema pamoja na mafanikio kadhaa  wananchi katika nchi za Afrika Mashariki  wanakabiliwa na changamoto  ya kupata  ajira na mazingira mazuri katika nchi hizo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati wa akifungua mkutano wa kujadili changamoto na fursa zinazopatikana kwenye nchi za Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.

Dk Sezibera  amesema mbali na ugumu wa ajira kwa wananchi kufanya kazi nchini nyingine  pia kuna mazingira magumu yasiyorizisha ya kufanya biashara yanayosababishwa na urasimu kwenye nchi wanachama.

Alisema wafanyabiashara wanawajibu wa kuzishawishi nchi zao kuweka mazingira mazuri kwani uchumi wa nchi unategemea sekta binafsi.

Awali Mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki(EABC)Felix Mosha alisema jitihada za makusudi zinatakiwa zichukuliwe ili kurahisisha mazingira ya kufanya biashara kwenye nchi za Afrika Mashariki.

Mosha alisema pamoja na vizuizi vya barabarani kupungua ipo haja  ya nchi wanachama kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya kuondosha vikwazo vya kibiashara ambavyo vinazorotesha uchuni wa EAC.


Mkutano huo ulidhaminiwa na benki ya KCB ambayo imefungua matawi kwenye nchi wanachama wa EAC ambazo ni Tanzania,Kenya,Rwanda,Burundi,Uganda na Sudan Kusini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...