Pages

May 13, 2014

ANGALIA PICHA HELKOPTA ILIYODONDOKA NCHINI KENYA NA KUUA 1 PIA KUJERUHI 11


Kamanda wa Polisi Kaunti ya Mandera kaskazini mwa Kenya amesema kuwa, mtu mmoja amefariki dunia na wengine kumi na moja kujeruhiwa vibaya baada ya helkopta ya jeshi la nchi hiyo KDF kuanguka katika eneo la makazi ya raia. 
Kamanda Noah Mwavanda amesema kuwa, helkopta hiyo ilikuwa imewabeba wanajeshi kutoka eneo la Elwak na kuwapeleka katika mji wa Garissa. 
Kamanda Mwavanda amesema kuwa, rubani wa helkopta hiyo amefariki dunia na wanajeshi majeruhi wote wamepelekwa kwenye hospitali ya Elwak kupata matibabu. Taarifa zinasema kuwa, serikali ya Kenya inajaribu kuongeza nguvu za kiulinzi kwenye maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Somalia kutokana na kuongezeka operesheni za kigaidi zinazosadikiwa kufanywa na wanamgambo wa kundi la al Shabab katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...