Kiongozi wa kundi la Boko Haram
Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa
nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya
Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo,
kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika
kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
No comments:
Post a Comment