Na Magreth
Kinabo
Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Seif Rashid amesema zaidi ya 35,000 hufariki dunia kila mwaka
kutokana na ugonjwa wa saratani.
Kauli hiyo imetolewa leo na
waziri huyo wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Saratani Duniani ambayo
huadhimishwa kila mwaka Februari 4 kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara
hiyo.
Aidha Dk. Rashid katika
kuaadhimisha siku kutoa upimaji Februari 4 na 5, mwaka huu bure, hivyo
aliitaka jamii kujitokeza mapema ili kupima ugonjwa
huo.
Alisema huduma za ugonjwa
huo ni haki ya kila mtu na matibabu yake ni bure.
“Hapa Tanzania tatizo la
Saratani limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka. Kila mwaka jumla ya wagonjwa
wapya wa Saratani 44,000 hugundulika na zaidi ya 35,000 hufariki kutokana na
ugonjwa huu,” alisema Dk. Rashid.
Aliongeza kuwa takwimu za
Taasisi ya Saratani Ocean Road, zinaonyesha kwamba kila mwaka inapokea wagonjwa
wapya wa Saratani 5,000. Wagonjwa hao wanakuja wakati Saratani ikiwa katika
kiwango cha juu - yaani hatua ya 3 na 4; na inasababisha uponaji wake kuwa
mgumu.
Kauli mbiu ya maahimisho ya
siku ya Saratani kwa mwaka huu ni “Kupunguza unyanyapaa na kuondoa dhana potofu
kuhusu Saratani”.
Aidha Dk. Rashid alisema
saratani inayoongoza hapa nchini kwa wanaume ni Saratani ya Kaposi na Saratani
ya Tezi Dume imekuwa ikiongezeka , na wanawake, Saratani ya Shingo ya
Kizazi.
Serikali katika kuboresha
imeanzisha huduma hizi katika Hospitali ya
Bugando, baadae
itaanzishwa katika Hospitali za Rufaa za KCMC na Mbeya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Twalib Ngoma alisema utafiti uliofanywa
unaonesha kuwa tumbaku huchangia wagonjwa wa saratani kwa asilimia 40 .
No comments:
Post a Comment