Taarifa za uhakika kutoka mjini Mugumu Wilayani Serengeti zinapasha kuwa diwani wa kata ya Stendi Kuu Mwalimu MARWA RYOBA (CHADEMA) ameswekwa ndani kwa amri ya mkuu wa wilaya.
Kadhia hiyo imemkumba diwani huyo ambaye pia ni maarufu sana mjini Mugumu kwa juhudi zake na ujasiri wake wa kutetea maslahi ya wananchi wa kata yake, wananchi wa mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu pamoja na wilaya ya Serengeti kwa ujumla. Diwani huyo ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Serengeti pia ametangaza nia ya kugombea ubunge mwaka 2015 na amekuwa akifanya mikutano maeneo mbalimbali wilayani humo akihimiza ujenzio na uimarishaji wa Chadema.
Baada ya kumalizika kwa vikao vya baraza la madiwani wilaya ya Serengeti Diwani Mwalimu Ryoba aliona ni busara kufanya mrejesho kwa wapiga kura wake juu ya mipango ya halmashauri kuhusu kata yao.
Katika mikutano hiyo iliyofanyika katika vitongoji vya Kyabakari,Chamoto na Bomani, diwani alikuwa akisikiliza na kupokea kero mbalimbali za wananchi. Mojawapo ya kero kubwa ambayo wananchi waliilalamikia ni zoezi la ukamataji wa mifugo hasa ng'ombe, zoezi linaloendeshwa na migambo wa mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu. Niwafahamishe tu kwamba mamlaka ya mji mdogo Mugumu ndiyo yameanzishwa hivi karibuni na vitongoji vilivyomo katika kata ya Stendi kuu inayounda sehemu ya mji mdogo wa Mugumu wakazi wake wengi takribani 95% ni wafugaji.
Katika malalmiko hayo ya wananchi wakabainisha kuwa migambo hao wamekuwa wakivizia mifugo katika maeneo yasiyozuiliwa na kuwakamata kasha mtendaji wa kata anawatoza faini, Jambo la ajabu ni kwamba mtendaji huyo amekuwa akiwapatia risiti za bandia ambazo hazina alama yoyote ya kuthibitisha kuwa ni risiti halali (nimeweka kiambatanisho).
Baada ya kusikiliza kero hiyo diwani Ryoba aliwataka wananchi wampe taarifa mara tu migambo watakapokamata mifugo yao na kuahidi kuwa suala hilo angelifuatilia kwa mtendaji wa kata na Mkurugenzi wa halmashauri. Alipokwenda kumhoji mtendaji na kumtaka aeleze ni kwanini anawakatia wananchi risiti feki ndipo zengwe lilipoanzia kwa mtenadji huyo kupeleka malalamiko kwa mkurugenzi kuwa diwani amemzuia kufanya kazi yake.
Siku mbili baadae Polisi wa kituo kikuu cha Mugumu mjini walimpigia simu diwani wakimtaka afike kituoni hapo. Diwani aliitikia wito na kufika polisi Mugumu kama alivyoitwa na alipofika kwa OCS akawekwa chini ya ulinzi na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi na kutishia uvunjifu wa amani.
Baada ya kufikishwa mahakamani tarehe 20/01/2014 na kusomewa mashitaka yake ya uchochezi na kutishia uvunjifu wa amani, polisi waliweka pingamizi la mshitakiwa kutopewa dhamana kwa madai kuwa kama akipewa dhamana ataingilia upelelezi na kwamba mtuhumiwa mwingine mmoja alikuwa bado hajakamatwa, na hivyo basi kesi imeahirishwa hadi tarehe 03/02/2014 itakapotajwa tena.
Baada ya makamanda kufuatilia kwa undani toka chanzo cha uhakika kutoka polisi Mugumu imebainika kuwa Diwani mwalimu Ryoba amekamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ikiwa ni njia ya kumkwamisha kisiasa kwakuwa diwani huyo anatishia kabisa nafasi ya ccm kushinda Ubunge Serengeti na hata kuongoza halmashauri ya wilaya na mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu.
Kwa wale waliopo Mugumu wanaweza kumtembelea kamanda Ryoba katika mahabusu ya Mugumu Mjini iliyopo karibu kabisa na hospitali teule ya wilaya, Mugumu DDH.Chanzo JF
January 25, 2014
Diwani wa CHADEMA Aswekwa ndani kwa Amri ya Mkuu wa Wilaya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment