Pages

September 29, 2013

VYOMBO VYA GWAJIMA VYAWA GUMZO VIWANJA VYA RELI ARUSHA, AANZA MKUTANO

Maandalizi yakiwa hatua za mwisho kukamilika .
Ikiwa unatazimiwa kuanza rasmi mkutano mkubwa wa kiroho katika viwanja vya reli mkoani Arusha utakaoongozwa na kanisa la Ufufuo na Uzima chini ya askofu Jospehat Gwajima kiongozi wa kanisa hilo, tayari hapo juzi wakazi wa eneo hilo na jirani walianza kukusanyika viwanjani hapo baada ya kusikia muziki wa kanisa hilo utakaotumika ukijaribiwa.

Kati ya watu waliosogea karibu ni pamoja na watumishi kutoka makanisa mbalimbali mkoani humo ambao hawakuacha kusema kwa muziki waliouona uwanjani hapo basi watu wataokoka kupitia muziki, ukiacha watumishi hao pia watu mbalimbali walionekana kujipanga wakiangalia ukubwa wa vyombo hivyo ambavyo vimening'inizwa kwenye vyuma maalumu na kujipanga sawia.

Kanisa hilo linafanya kwa mara ya kwanza mkutano mkubwa wa injili mkoani Arusha ambao ulianza siku ya  tarehe 27 mpaka tarehe 10 mwezi ujao ukiwa na waimbaji mbalimbali akiwemo Flora Mbasha, John Lisu, Jackson Benty, Maximilian Machumu a.k.a Mwanamapinduzi, kundi la sifa na kuabudu la kanisa hilo wakifahamika kama Platform pamoja na waimbaji wengine, kisha mkutano huo utahamia mkoani Kilimanjaro.

Ufungaji vyombo ulipoanza, hapa vikishushwa kutoka katika malori yanayomilikiwa na kanisa hilo.
Vyombo vilipokuwa vikipandishwa.
Baadhi ya watumishi waliovutwa na kishindo cha muziki uwanjani hapo.
Baadhi ya mabasi ya kanisa hilo yakiwa yamepaki jijini Arusha.
Watu wakiwa wamejitokeza barabarani kusikiliza matangazo ya mkutano huo kupitia gari la matangazo. Picha zote kwahisani ya Ufufuo na Uzima.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...