MAJANGILI waanza kuua ndege TAI, wawawekea sumu kwenye mizoga ya tembo ili kukomesha tabia yao ya kutoa 'ALERT'.
Mauaji ya tembo yanayoendelea katika nchi mbalimbali barani Afrika yamefikia katika kiwango cha kutisha 'at a point of no return' na ubaya kila kukicha majangili wanakuja na mbinu mpya za kuhakikisha wanatekeleza azma yao.
Baada ya kugundua kuwa wale ndege tai wanatoa taarifa kwa askari wa wanyama pori, (tai wakiona mzoga huwa wanazunguka maeneo hayo) wameanza kuwaua ndege hao kwa kuwawekea sumu katika mizogo ya tembo.
Tai ambao hupenda kuambaa ambaa angani wakizunguka eneo palipo na mzogo wameonekana ni kero na watibuaji wakubwa wa njama za majangili ambao hufanya shughuli zao mchana kweupe.
Tai hukusanyika katika makundi makubwa ili kuweza kupata chakula kwa kupambana na wanyama kama simba, fisi nk, na kama hali hii itaendelea kuna hatari hata wanyama wengine wala nyama wakiwemo akina fisi, nao wakapoteza maisha.
Katika tukio moja lililotokea huko Botswana tai zaidi ya 600 walikufa baada ya kula sumu iliyowekwa kwenye mzoga wa tembo, hata hivyo hakuna uhakika kama mamlaka zetu hapa nchini zinataarifa ya mauaji haya ya tai katika hifadhi zetu nchini.
No comments:
Post a Comment