Padri
Joseph Magamba akiwa wodini akipatiwa matibabu. ZANZIBARI.
PADRI wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph Monesmo Magamba amemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege jana jioni.Mkoa wa Mjini Magharibi,Zanzibar.
PADRI wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph Monesmo Magamba amemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege jana jioni.Mkoa wa Mjini Magharibi,Zanzibar.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Hana alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba kiongozi huyo wa dini amelazwa katika Hospitali ya Mnazi
Mmoja, akiendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa usoni, kifuani na
mikononi.
Hana
alisema kwamba Padri Magamba (60) alikuwa akitokea katika duka la huduma za
mawasiliano ya mtandao la Shine Shine saa 10.15 jioni na watu waliommwagia
walimtega mlangoni kabla ya kufanya uhalifu huo na kutoweka kwenye vichochoro
vya Mitaa ya Mtendeni na Mchangani.
Alisema
polisi wamestushwa na tukio hilo kwa vile limetanguliwa na matukio matatu ya
kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano
wa kufanikisha kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo
hivyo.
“Tumeanza
kufanya uchunguzi ikiwemo kuchukua maelezo ya majeruhi, tungependa zaidi kupata
msaada wa kitaarifa kwa watu walioona na wanaojua mahali walipo watu wanaofanya
vitendo hivyo,” alisema Hana.
Mfanyakazi
wa Duka la Huduma za Mawasiliano ya Mtandao, Rukia Yahya Abass alisema
anamtambua Padri Magamba kama mteja wake wa muda mrefu na huja dukani hapo
nyakati za asubuhi au jioni kwa ajili kupata huduma za
mawasiliano.
Rukia
alisema ameshtushwa kuona padri huyo baada ya kumaliza kupata huduma na kutoka
nje akipiga mayowe ya kujeruhiwa.
“Nimezoea
kumwita father au babu, ni mteja wangu kwa kweli, nilimwona akirudi tena ndani
huku akiomba msaada, watu waliokuwa katika mtandao harakahara wakammwagia maji,
alikuwa akilalamika kwa ukali wa maumivu,” alisema Rukia akiwa na
huzuni.
Alisema
wasamaria wema ndiyo waliomchukua na kumpeleka hospitali. Kabla ya tukio hilo
alilipa gharama za huduma ambazo zilikuwa ni Sh2,000 na kurudishiwa chenji yake
baada ya kutoa noti ya Sh10,000.
Daktari
Jamal Adam ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja alisema
kwamba Padri Magamba amepatiwa huduma ya kwanza na anaonekana amejeruhiwa usoni,
mikononi na kifuani.
“Ni mapema
mno kusema ameathirika kwa kiasi gani kutokana na tukio hilo, tunaendelea na
juhudi za kumtibu, ”alisema Dk Jamal.
Huu ni
mfululizo wa visa vipatavyo vinne vya kikatili ambavyo vimefanyika Zanzibar,
vikiwalenga watu maalumu katika kipindi cha miezi 10 iliyopita. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment