Pages

September 7, 2013

BONANZA LA TASWA KUFANYIKA ARUSHA KESHO


Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo(Taswa Arusha) Mussa Juma akizungumza na vyombo vya habari
 kuhusu Bonanza la waandishi linalotarajiwa
kufanyika kesho jumapili katika kiwanja cha General Tyre.




Tamasha la michezo la waandishi wa habari Taswa linatarajia kufanyika
kesho September nane katika viwanja vya general tyre  vilivyopo njiro
jijini hapa.

Akiongelea tamasha hilo katibu wa chama cha waandishi wa habari za
michezo mkoani arusha Musa Juma alisema kuwa maandalizi ya tamasha
hilo yamekamilika na jumla ya timu 12 zinatarajiwa kushiriki katika
tamasha hilo.

Alisema kuwa michezo mbali mbali itachezwa katika tamasha hili ikiwa
ni pamoja na kufukuza kuku,kukimbia na magunia,mpira wa miguu ,mpira
wa pete pamoja na michezo mingine mbalimbali sambamba na burudani
mbalimbali za muzikikutoka katika sehemu na bendi mbalimbali.

Alisema kuwa hili nitamasha la nane kufanyika na kwa mara hii
wameboresha zaidi kwani zawadi zimeongezeka tofauti na kipindi
kingine.

Amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza katika tamasha hili  kwani
tamasha hili ni lakihistoria  kutoka na waandishi mbalimbali kushiriki
kutoka katika mikoa mbalimbali.

Alitaja baadhi ya timu zitakazo shiriki katika tamasha hili kuwa ni
pamoja na timu ya taswa ya jijini dar es salaamu ambapo inatarajiwa
kuwasili leo timu ya taswa arusha ambao ni wenyeji wa bonanza
hili,timu ya taswa manyara ,timu ya triple a fm ,sunrise fm,radio five
pamoja na timu nyingine nyingi ikiwemo timu ya tbl ambao ni wathamini
wakuu pamoja na timu ya wazee klabu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...