Moja ya tanki linalopeleka maji katika kijiji
cha Mbatakero
Na
Mwandishi Wetu Hai
Wilaya ya
Hai itakamilisha ufikishaji wa maji safi na salama katika vijiji vitano kupitia
mkakati wa sasa wa serikali wa Mfumo mpya unaolenga kuleta mapinduzi ya kijamii
nchini wa usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo unaojulikana kama
matokeo makubwa sasa yaani “Big Results Now” ifikapo Septemba 30 mwaka
huu.
Vijiji
hivyo vitano kati ya kumi ambavyo kwa kila Halmashauri nchini itahakikisha
vinaingizwa katika mpango wa kupata huduma ya maji safi na salama ni
Mbatakero,Ngosero,Kwasadala,Kimashuku na Kwatito ambavyo vitaunganishwa na maji
safi na salama ya Bomba kutokea katika Skimu ya Lyamungo-Umbwe.
Mkuu wa
wilaya ya Hai,Novatus Makunga akizungumza katika mikutano mbalimbali ya vijiji
vya Ngosero na Mijongweni mwishoni mwa wiki ameeleza kuwa maji hayo yatafika kwa
umbali wa kilometa 22.73 na utekelezaji wa kazi umefikia asilimia
85.
Ameanisha
kazi ambazo tayari zimeshakamilika ni pamoja na ujenzi wa chemba ya kuchukulia
maji,ujenzi wa kivuko kutoka mto kikafu,ujenzi wa matanki mawili ya lita za
ujazo 50,000 kila moja,ujenzi wa vilula 20,kuchimba mtalo kilometa 21,kulaza na
kufukia mambomba kilometa 20
Amewahakishia
wananchi wa vitongoji viwili ambavyo viliachwa katika mradi huo vya Landi na
Jitengene katika kijiji cha Ngosero nao watapata maji ifikapo mwishoni mwa mwezi
Septemba
Amefafanua
kuwa katika mpango huo kijiji cha Kimashuku kitahusu vitongoji vya Kinyalu na
Kiangaa,Kijiji cha Kwasadala kitongoji cha Faraja na kijiji cha Kwatito ni
kitongoji Kasendero
Amesema
kukamilika kwa mradi huo kutaweza kupatikana kwa huduma ya maji kwa wakazi zaidi
ya 3,443 katika umbali uziozidi mita 400.
Makunga
amesema baada ya kukamilika kwa awamu hiyo ya kwanza,serikali wilayani humo
itaanza mara moja utekelezaji wa awamu ya pili ya upelekaji wa maji katika
vijiji vitano ambayo inatakiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni
mwakani.
Ametaja
vijiji vitakavyohusika na awamu ya pili kuwa ni pamoja na Sanya
Stesheni,Chemka,Mtakuja na Tindigani pamoja na mji wa Bomang’ombe kupitia Skimu
ya maji ya Losaa-Kia
“Hivi
vijiji vya awamu ya pili vilikuwa na tatizo kubwa sana la maji kwa muda mrefu
kutokana na kukosa kabisa chanzo chochote chenye maji safi na salama kutokana na
maji ya maeneo hayo kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya floride ambayo yamekuwa
na athali kubwa kiafya kwa watumiaji na hasa watoto
wadogo,”amefafanua
Akifafanua
kuhusiana na mji wa Bomang’ombe,Makunga ameeeza kuwa hivi sasa unakabiliwa na
uhaba wa maji kutokana na ongezeko kubwa na la kazi la watu kutokana na wenyeji
wengi wa mji ya Moshi,Arusha,Mererani na Sanya juu kupenda kuweka makazi yao
katika mji huo.
Ameeleza
kuwa mji wa Bomang’ombe unaopata maji kutoka skimu ya Uroki-Bomang’ombe
ilisanifiwa kwa kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wapatao
10,000.
Kutokana
na ongezeko la wakazi wa mji wa Bomang’ombe na kufikia 34,000 kwa sasa,huduma ya
maji safi na salama katika mji huo haikidhi matumizi kwa wakazi kwa
siku.
Maeneo
yenye upungufu wa maji katika mji huo ni Bomani juu na hususani hospitali ya
wilaya ambayo kwa kipindi cha kiangazi inapata huduma ya maji wakati wa usiku
tu.
No comments:
Post a Comment