Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais
Jakaya kikwete.
Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe.
Diwani huyo, Dioniz Bugali
wa Kata ya Kamhanga, vilevile alimteua Diwani wa CCM kuhesabu kura
zake.
Bugali alifanya kituko
hicho mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Geita kwenye
mkutano wa nne wa baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Katika
uchaguzi huo wa makamu mwenyekiti wa halmashauri,mgombea wa CCM alikua Masoud Kimondo ambaye ni diwani wa Kata ya Kasema wakati wa Chadema alikua ni Bugali.
“Nimesimama hapa kuomba
kura…kabla ya kuomba kura naomba niseme neno…nafasi hii ya makamu mwenyekiti wa
halmashauri sikuwa naitaka isipokuwa nimelazimishwa na chama changu (CHADEMA)
kugombea.
“Nachotaka kusema hapa
ni kwamba nikishindwa sitakata rufaa.Ninampongeza sana mgombea mwenzangu wa
CCM, mimi hapa pamoja na kuwa ni diwani wa Chadema na ninagombea nafasi hii
kupitia chadema, lakini bado ni katibu mwenezi wa CCM kwenye kata yangu ya
Kamhanga…nipeni kura zenu,”alijinadi Dionizi baada ya kupewa nafasi kuomba
kura.
Kauli hiyo ilisababisha
madiwani wa CCM kulipuka kwakicheko wakidai Bugali ni mwenzao na wengine
wakiitambia Chadema kwa kusema, “Haloohalooooooooooooooo … Chadema
mmesikiaaaa…hiyo ndiyo CCM…Spidi 120…Chadema hamna chenu Kamhanga huyo ni
mwenzetu.”
Pia baada ya kura
kupigwa diwani huyo wa Chadema alimteua Diwani wa CCM Kata ya Nkome, Karema
Chiratu kuwa wakala wake wa kuhesabu kura huku madiwani wenzake wanne wa Chadema
wakibaki mdomo wazi.
Akisoma matokeo hayo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Lupuga, alimtangaza Kimondo kuwa
mshindi kwa kupata kura 29,dhidi ya Bugali aliyepata kura mbili.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
No comments:
Post a Comment