Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkaoni Arusha,Joshua Nassari(kulia)akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema.Picha na Filbert Rweyemamu
Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nassari amejisalimisha leo kwenye kituo kikuu cha Polisi mkoani Arusha kuhojiwa juu tuhuma za kumshambulia mkazi wa Makuyuni wilayani Monduli mkoa wa Arusha,Hussein Warsama wakati uchaguzi wa madiwani uliofanyika mwezi uliopita.
Katika tukio hilo Mbunge huyo alijeruhiwa nakulazwa katika hospitali ya Selian na baadaye kukimbizwa kwa ndege ya kukodi kwenda kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi,akiwa anapata matibabu aliwalaumu viongozi wa kisiasa kuhusika na tukio la yeye kutekwa na kuumizwa.
Wakati wa tukio hilo,Kamishna wa Polisi anaehusika na Operationi na Ufatiliaji aliwaambia waandishi wa habari kuwa Mbunge huyo anapaswa kijisalimisha kujibu tuhuma za kumshambulia Hussein Warsama.
Nassari alisema baada ya mahojiano hayo aliondoka kituoni hapo na kuendelea na shughuli zake za kuwatumikia wananchi wa jimbo lake. |
No comments:
Post a Comment