Pages

June 25, 2013

POLISI RUVUMA WAKAMATA MENO YA NDOVU YATANGAZA KIAMA KWA MAJANGIRI


Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma ,Deusdedit Nsimeki akipanga meno ya Ndovu kulingana na uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake .

 

JESHI  la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya ndovu 18 yenye uzito wa kilo 84 yenye  thamani ya Shilingi 216 Milioni  sawa na dola 15 elfu za Kimarekani. Kwa meno hayo ni sawa sawa na Tembo tisa waliouwawa  kikatili kisa kumiliki meno hayo yanayohitajika na majangiri wasio na huruma na viumbe hivyo vilivyobeba meno yenye thamani kubwa.
 
 Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma,  Deusdedit Nsimeki, amesema kuwa tukio hilo la kukamata meno hayo lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku  katika Kijiji cha Majala Kata ya Nandembo wilayani Tunduru.
  
 Kamanda Nsimeki, amesema kuwa  tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo lilitokea  baada ya askari Polisi wa wilaya hiyo kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa ambao kwa bahati mbaya hawakukamatwa.
   
  Tukio hilo limekuwa  la pili la  katika kipindi  kifupi lile la kwanza  lilitokea katika kijiji  cha Hanga wilayani Namtumbowsiki mbili zilizopita
  
  Kamanda Nsimeki ametangaza kiama kwa majangiri mkoani Ruvuma na amewataka wajisalimishe la sivyo watakiona cha mtemakuni.
"jeshi la polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao wamejificha na wanajihusha na matukio hayo ya ujangili kwa wanyama  na hasa tembo" alisema Nsimeki.
             
Pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo vya uhalifu wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi na wananchi.

Chanzo:Jamii ya Wana Ruvuma

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...