Longido,Arusha
Shughuli za biashara na watu kusafiri kupitia mpaka wa Namanga,wilayani Longido mkoani Arusha uliopo mpakani kati ya Tanzania na Kenya bado zinasuasua kutokana na uchaguzi uliofanyika hivi kariburini.
Uchunguzi wa Mwananchi jana ulibaini kuwepo kwa watu wachache wanaoingia na kutoka Kenya tofauti na ilivyo kawaida kwa mpaka huo kuwa na shughuli nyingi.
Dereva mmoja wa gari linalofanya safari zake kutoka Namanga hadi jijini Arusha,George Mollel alisema siku chache kabla ya uchaguzi idadi kubwa ya Wakenya wenye asili ya nje na Watanzania walipitia mpaka huo kuingia nchini kwa wingi.
“Hata Wakenya wengi walienda kwao kupiga kura,kama unaovyoona wanaanza kurudi mmoja mmoja kwenda kwenye mikoa mbalimbali kwenye kazi zao,kwakeli hali ya biashara sio nzuri kwa sasa”alisema
Alisema baada ya uchaguzi kwa siku tatu hapakuwa na magari ya abiria yaliyokuwa yanaenda Kenya wala kutoka huko ila baada ya matokeo kutangazwa magari ya abiria yameanza kuonekana.
Jitihada za kumpata Afisa Uhamiaji katika kituo hicho,Albert Kishe hazikufanikiwa kwa maelezo kuwa yupo kwenye matibabu na Afisa aliyekuwepo zamu, Ally Said hakuweza kutoa takwimu za wasafiri kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo.

إرسال تعليق