DK.MIGIRO: YALIYOTOKEA YAMETIA DOA, LAKINI TUMEVUKA NA TUMEBAKI KUWA TAIFA MOJA


Na Said Mwishehe,Michuzi TV


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiroameweka wazi kuwa vurugu zilizotokeaOktoba 29 mwaka 2025 zimetia doa katikataifa la Tanzania lakini limeweza kuvukakipindi kile na kubaki kuwa Taifa moja.

Dk.Migiro ameyasema hayo alipokuwa ajibu maswali ya mtangazaji wa Crown Media Salim Kikeke aliyekuwa akifanya mahojiano maalumu na Katibu Mkuu huyo kuhusu hali ambayo Taifa limepitia baada ya vurugu za Oktoba29.

Katika swali lake Kikeke alisema kuna watu kutoka vyama vya vingine na wengine kutoka ndani ya CCM wanazungumza mambo ambayo ukiyatazama unaona kimsingi kama yanaligawa Taifa badala ya kulileta pamoja, hivyo akataka kujua msimamo wa Chama Cha Mapinduzi katika hilo

“Pamoja na kwamba wapo wanaopazasauti hizo lakini ukweli ni tumebaki kuwataifa moja, tumeendeelea kuendeshashughuli zetu za kiuchumi na kijamii bilakutetereka ndani muda mfupi,amani ilirejea,uchumi wetu bado umebaki tulivu natunajua duniani kuna vyombo vya kupima,kutathimini ukuaji wa uchumi.

Vyombo vyote vimeeleza hata baada ya kadhia ile ya Oktoba 29 uchumi wetu umebaki tulivu.

“Hii inaonesha sio tu ustahimilivu ,inaonesha tumeendeelea kuwa taifa mojatukiwa na njia moja ya kujijenga kijamii nakiuchumi lakini utaona hali hii ya umoja nautulivu haipimwi tu na sisi wa ndani au Chama Cha Mapinduzi .Tumeona baada yatukuo lile bado watu wameendelea kuwa naimani na taifa hili, wameendeelea kuonautulivu wetu umerejea.”

Akiendelea kujibu Dk.Migiro amesema Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi aliwapokea wawekezaji kutoka mataifa matano.Pia taifa limepokea wafanyabiashara kutoka Urusi huku akiongeza China pia imeendelea kuwekeza.

“Nasiku za karibuni Mwakillishi Mkazi wa Kanda hii wa Benki ya Dunia alikwenda kumuaga Rais wetu baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi katika kanda hiina alimueleza kuwaTanzania bado inamaoteo mazuri ya kukua kwa uchumi.

“Kwahiyo siamini kama tungekuwa ni taifalililogawanyika haya yote yangetokea nawapo tumewasikia wanaosema taifalimegawanyika ,limepasuka.Chochote wanachokiona ambacho ni kiashiria cha kugawanyika au kiashiria cha mpasuko Mtanzania yeyote ambaye ana mapenzi mema na taifa letu atakuwa na sauti ya kuunganisha ,sio sauti ya kuleta mpasuko na hili linakuwa na umuhimu zaidi kwa watukama sisi viongozi .

“Nimewahi kuwa kiongozi kwa nafasi yangundogo mpaka ngazi ya Uwaziri. Kitaifanimepata heshima kubwa ya kufanya kazinyingine katika taifa letu ,nilikuwa mpaka Julai mwaka jana nilipata heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kitalaam ya uandishi wa Dira ya Taifa 2050 .Niheshima kubwa na ni sehemu ya uongozi ambaonilipata heshima ya kuwa nayo.

“Kwa maana hiyo ninapozungumza lazimakauli yangu iakisi dhamana na heshimaniliyopewa ya kuwa kiongozi .Sauti yangukama kiongozi au viongozi wengine wawewakijamii , dini au kisiasa. Kiongozi wakweli ni yule anayepaza sauti ya kukubalikuna kitu kilitupata lakini kusema kwamba tusiendelee kukaa kwenye kadhia hii kwa namna ya kuendeleza mpasuko,”amesema Dk.Migiro na kusisitiza hakuna mgawanyiko.

Pia amesema viongozi wanawajibu wakuhakikisha wanaendelea kwa kauli zetu navitendo vyao kushikamana kama taifa nakuimarisha umoja wetu .

Kuhusu ripoti ya Jaji Chande kuwa walibainiuwepo wa picha za akili unde ambazozilitizamwa na kuna madai pengine kunapicha zinasingiziwa akili unde ili kufichayaliyotokea Oktoba 29 na nini maoni yaCCM

Dk.Migiro amejibu kuna picha ambazo akiliunde lakini kuna picha ambazo ni za matukio ya zamani zimeunganishwa namatukio ya Oktoba 29 na tume imeelezaziko picha ambazo ni za matukio yasehemu nyingine nje ya nchi lakinizimeunganishwa.

“Sasa tume ilipokuwa inaeleza metholodojia iliyotumia ilisema \wametumia watalaam wautambuzi kutambua zile picha ni za lini ,zawapi na za wakati gani. Hayo ni masuala yakitalaam .Mimi na wewe ndugu Kikekesidhani kama tuna nafasi kubwa yakuzungumzia utalaam wa aina hii.

“Wewe mwenzangu ni mtalaam wa mambo ya habari kama hivi unavyonihoji .Mimi ninataaluma yangu ndogo ya sheria lakini sikusomea sheria ya utambuzi .Nadhani itakuwa vema na busara tukawaachia watalaam wakachambua hili na tunaamini baada ya Tume ya Upelelezi wa Jinai kumaliza kazi yake tutapata mwanga zaidi kuonesha mambo zaidi yalikuaje Oktoba 29 na baadae nini kilitokea,”amesemaDk.Migiro.

Post a Comment

Previous Post Next Post