KAMPUNI YA MAWASILIANO YA YAS YAZINDUA CHAPA YAKE MKOA WA ARUSHA

Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Joseph Mkude akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa chapa ya Yas na Mixx by Yas  kwa wakazi wa mkoa wa Arusha.
 
Wakazi wa mkoa wa Arusha walioshiriki hafla ya chakula jioni kutambulisha chapa mpya ya Yas katika hoteli ya Mount Meru.
Wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na mawakala walioshiriki hafla hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Mawasiliano ya Yas, Kanda ya Kaskazini,Daniel Mainoya akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa chapa ya Yas na Mixx by Yas iliyofanyika jijini Arusha.

Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Yas, Kanda ya Kaskazini,Daniel Mainoya(wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya Arusha,Joseph Mkude wakati wa uzinduzi huo ,kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Mixx by Yas,Justino Lawona na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa(Yas Business),Antony Lelo.

Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Mawasiliano ya Yas, Kanda ya Kaskazini,Daniel Mainoya akizungumza wakati wa hafla hiyo,kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano Mixx by Yas,Justino Lawona na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa,Antony Lelo.


Na Mwandishi Wetu,Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Joseph Mkude amezindua Chapa ya kampuni ya mawasiliano ya Yas na Mixx by Yas mkoani hapa na kusisitiza umuhimu wa teknolojia katika kurahisisha mawasiliano kwa njia ya kidijitali na huduma za kifedha.

Katika uzinduzi huo uliwaleta pamoja watumiaji wa mawasiliano wa mtandao huo kutoka taasisi za umma,binafsi na mawakala wakubwa kupata uelewa wa maboresho tangu kuanza kwa chapa mpya kutoka ya zamani ya Tigo.

Mkude amesema kwa miaka mingi teknolojia imeendelea kubadilisha maisha ya watanzania  na kuongeza fursa za kiuchumi hapa nchini.

"Kupitia uzinduzi wa chapa hizi mbili  Yas na Mixx by Yas tunashuhudia  si tu mageuzi ya kimuonekano,bali ni mageuzi ya kimtazamo,mbinu,dira katika kutoa huduma bora zinazogusa maisha ya kila mtanzania kwa namna ya kipekee"amesema Mkude

Ameongeza kuwa Yas na Mixx by Yas wanakuja na suluhisho la kweli la maisha ya kila siku  jambo ambalo ni mchango mkubwa kwa juhudi za serikali ya awamu ya Sita katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma bora za kifedha na mawasiliano bila kujali mahali walipo.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kaskazini,Daniel Mainoya amesema kwa miaka 30 Tigo imekua kinara wa mageuzi ya kidijitali ikiwaunganisha watanzania  na kuwapatia  fursa za kifedha kupitia teknolojia,tunasonga mbele tukiwa na chapa mpya ya Yas,Yas si chapa mpya tu bali falsafa ya mabadiliko,uvumbuzi na mshikamano wa kiuchumi.

"Yas ni mwelekeo mpya wa kidijitali,ni chapa inayolenga kwezesha vijana,wafanyabiashara wadogo na wa kati na kila mtu anayetafuta fursa za kujikwamua kupitia teknolojia na huduma za kifedha,"amesema Mainoya.

mwisho


Post a Comment

أحدث أقدم