Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Erick Mvati, akizungumza alipokutana na Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Afisa Masoko Mwandamizi, Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS, Bw. Rahim Mwanga, akiwafungulia akaunti ya uwekezaji watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.

Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wakifuatilia mada mbalimbali ikiwemo akiba, mikopo, uwekezaji, bima, kujiandaa kustaafu wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.

Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akiteta jambo na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, baada ya kumalizika kwa mafunzo ya elimu ya fedha kwa watumishi hao yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.

Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, akitoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Taasisi zake.
إرسال تعليق