Filbert Rweyemamu
Arusha.Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) imethibitisha matumizi ya mtaala
unganishi wa masomo ya ufundi nchini utakaowawezesha wahitimu wa vyuo
vya Mafunzo ya Ufundi Stadi(Veta) kuendelea na elimu ya juu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mtaala huo,Mkurugenzi wa Ufundi na Mafunzo ya
Ufundi Stadi nchini,Dk Noel Mbonde amesema utasaidia kuwapa fursa vijana
wengi waliotamani kuendelea na masomo ya ufundi ya juu kunufaika.
Amesema
serikali inathamini maboresho hayo yanayotoa nafasi ya kuwanoa
wataalamu wa kutosha inayoenda sambamba na sera ya serikali ya awamu ya
tano ya kufikia uchumi wa viwanda.
"Kulikua na
tatizo la wanafunzi wetu wanaohitimu Veta kuendelea na kozi za juu za
ufundi na sababu kubwa ilikua ni kukosekana kwa sifa za kuwawezesha
kujiunga na kozi za ufundi katika ngazi ya Stashahada na kuendelea
mtaala unganishi umekua jibu,"alisema Dk Mbonde
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Erick Mgaya amesema mtaala huo
ni matokeo ya mahitaji ya wahitimu wengi wa vyuo vya Veta nchini kuwa
na shauku ya kuendelea na masomo ya juu ya ufundi.
Amesema
kwa ushirikiano wa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sault nchini Canada
walikamilisha mtaala huo unawapa sifa wanaotaka kuendelea na masomo kwa
kuhudhuria kozi maalumu kwa muda mwa miezi mitatu.
Naye
Mratibu wa NACTE Kanda ya Kaskazini,Godfrey Komba amesema mtaala huo
umekuja kwa wakati muafaka ambao serikali inahimiza matumizi ya
teknolojia katika kusukuma ajenda ya uchumi wa viwanda nchini.
Aliwataka
vijana kuchangamkia fursa hiyo ya kupata elimu unganishi inayowapa
nafasi ya kuendelea na elimu ya juu ya ufundi itakayofungua milango
zaidi kwa kutoa nafasi ya kupata ajira kwenye makampuni makubwa na
kujiajiri wenyewe.
Kwa upande wake Mshauri wa
Elimu ya Ufundi kutoka nchini Canada,Dk Allan Copeland amesema jumla ya
wanafunzi 72 wameanza kozi unganishi katika Chuo cha Ufundi Arusha
kutoka mikoa mbalimbali ambao ni wahitimu wa vyuo vya Veta.
No comments:
Post a Comment