*Waziri Mwijage asema Taifa limepata pigo kubwa kwa kupoteza watumishi waadilifu.
*Mkurugenzi Mtendaji TIC aelezea utendaji wao, azungumzia namna alivyowaamini.
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
Ni
vilio na simanzi ndivyo vilivyokuwa vimetawala katika Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga miili ya watumishi wa tatu
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) waliofariki dunia kwa ajali ya
gari wakitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma kikazi.
Miili
hiyo ilifikishwa kwenye viwanja hivyo saa nne asubuhi leo ambapo mamia
ya waombolezaji walioongozwa na Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Charles Mwigaje.Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe
pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali Serikali.
Watumishi
hao wa TIC ambao miili yao imeagwa leo viwanjani hapo ni aliyekuwa
Mkurugenzi Idara ya Utafiti,Mipango na Mifumo ya Mawasiliano Said Amiri
Moshi, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za kitaasisi Zacharia Kingu Meneja
Utafiti Martin Masalu
Akizungumza
mbele ya mamia ya waombolezaji,Waziri Mwijage amesema vifo vya
watumishi hao ni pigo kubwa kwa TIC, Taifa na familia kwa ujumla na enzi
za uhai wao walikuwa vijana walioonesha umahiri mkubwa wa kiutumishi.
Amesema
kwake yeye watumishi hao walikuwa ni marafiki zake na anachoweza
kukilezea anatambua mchango wa kila mmoja wao kutokana na utendaji kazi
wa kizalendo waliouonesha kwenye kituo hicho.
Amesema waliaminiwa na kupewa majukumu makubwa hasa kwa kuzingatia walikuwa na uelewa mkubwa kuhusu masuala ya uwekezaji.
"Nikiri
vijana hao wameacha pigo kubwa kwetu hasa kipindi hiki ambacho tupo
kwenye mchakato wa ujenzi wa viwanda nchini.Hata hivyo vijana wengine
waliobakia TIC waendelea kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya nchi
yetu.
"Watumishi
hawa ambao leo tunawaaga walifariki wakiwa njiani kelekea Dodoma kwa
ajili ya kutekeleza majukumu muhimu.Tunafahamu kuna baadhi ya
changamoto ambazo zipo kwenye uwekezaji hivyo walikuwa wanakwenda
kwenye kikao kuwaambia watendaji wa Serikali mambo muhimu ya kuvutia
uwekezaji nchini,"amesema.
Amesema
wakati anapata taarifa hizo za msiba alipatwa na mshtuko na hakujua
afanye nini lakini kwa kuwa imetokea, kilichobaki watendaji wa TIC
kuendelea na ujenzi wa nchi yao huku akifafanua haina tofauti na vitani
askari mmoja akitangulia mbele ya haki basi waliobakia wanachukua silaha
wanatakiwa kusonga mbele kwani kinyume na hapo taifa litapata hasara.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Mwambe amesema vifo vya watumishi
hao ni pigo kubwa kwao hasa kwa kuzingatia ni walikuwa watumishi ambao
walitekeleza majukumu yao bila kuchoka na kutanguliza uzalendo kwa nchi
yao.
Amesema
watumishi hao hata pale ambapo alikuwa akipata safari za kikazi
hakusita kuwaachia ofisini kuendelea na majukumu ya kituo hicho na
kufafanua TIC imeamua kugharamia shughuli zote za mazishi ya watumishi
hao huku akielezea namna ambavyo wameumizwa na vifo hivyo.
Mwambe
ameelezea namna ambavyo watumishi hao kila mmoja kwa nafasi yake enzi
za uhai wao walivyokuwa muhimili na kiunganishi muhimu kwa wawekezaji wa
ndani na nje , hivyo wameacha pigo kubwa.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza
jambo kwa ndugu na jamaa wa marehemu wakati kuagwa kwa miili ya
watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kwenye ukumbi wa
Kareemjee jijini Dar es Salaam.
MkurugenziMtendaji
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe akizungumza na
mbele ya waombolezaji walioshiriki kuaga miili ya watumishi wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania(TIC) kwenye ukumbi wa Kareemjee jijini Dar es
Salaam.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole akitoa neo la pole kwa ndugu
na jamaa wa marehemu wakati wa kuagwa kwa miili ya wafanyakazi wa TIC.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akitoa heshima
ya mwisho kwenye miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania(TIC).
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola akiaga miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)
Katibu
wa Itikadi na Uenezi CCM Hamphrey Polepole akitoa heshima za mwisho
kwenye miili ya watumishi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Zamani wa TIC na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Morogoro, Clifford Tandari(katikati) akiaga miili ya wafanyakazi wa TIC.
Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wakitoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofariki dunia kwa ajali ya gari wakitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma kikazi.
No comments:
Post a Comment