Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Uamuzi
wa Serikali wa kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa
kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na benki za biashara nchini,
umechochea taasisi za fedha yakiwemo mabenki kuanza kupunguza viwango
vya riba ya mikopo hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi.
Hayo
yalisemwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Ashatu Kijaji wakati wa kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha
uliowashirikisha wabunge, washirika wa Maendeleo, wakuu wa Taasisi za
fedha na Wizara ya Fedha na Mipango.
Dkt.
Kijaji, alisema kuwa Serikali kupitia Benki Kuu imeshusha riba ya
mikopo kwa taasisi za fedha kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0 na
kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa katika Benki
hiyo na benki za biashara kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0
kuanzia mwezi Aprili 2017, jambo ambalo limeleta matokeo chanya katika
kuimarisha uwezo wa taasisi kukopesha wateja wao.
Miongoni
mwa Benki zilizoshusha viwango vyao vya riba za mikopo ni CRDB ambayo
imetangaza kushusha riba kutoka asilimia 22 hadi 16 na kuongeza kiasi
cha kukopa kwa wafanyakazi kutoka Sh. milioni 50 hadi Sh. milioni 100
huku muda wa kurejesha ukiongezwa kutoka miaka mitano hadi saba.
Benki
nyingine ni NMB ambayo imeongeza muda wa marejesho ya mikopo kwa
wafanyakazi, wajasiriamali wadogo na wakubwa kutoka miezi 60 hadi 72,
na imepunguza riba ya mikopo kwa wafanyakazi kutoka asilimia 21 hadi 19
na wajasiriamali wadogo kutoka asilimia 23 hadi 21.
Dkt.
Kijaji amezipongeza benki zilizoshusha viwango vya riba na ameitaja
hatua hiyo kuwa ni muhimu katika kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya
viwanda hata kabla ya mwaka 2025 na kutoa wito kwa taasisi hizo za fedha
kuitupia jicho sekta ya kilimo kutokana na umuhimu wake katika kutimiza
malengo ya kukuza viwanda.
Aidha,
Dkt. Kijaji alisema kuwa Serikali imekamilisha andiko “Blue Print”
ambalo lengo lake ni kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ili
kuleta tija kwa wafanyabiashara na Sekta ya Fedha kwa ujumla
Alisema
Serikali imeendelea kulipa malimbikizo ya madai mbalimbali
yaliyohakikiwa ya watumishi, wakandarasi na watoa huduma wengine
yaliyohakikiwa ili kuongeza ukwasi katika jamii na kwa kwamba uhakiki
uliofanyika umeokoa kiasi kikubwa cha fedha za Serikali ambazo
zingelipwa wakati madai hayakuwa sahihi.
Naibu
Waziri huyo aliipongeza Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kushiriki kwa
vitengo katika utekelezaji wa Mpango huo kwa kutekeleza miradi ya
kimkakati ya kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari katika eneo la
Mkulazi na Mbigiri - Morogoro na mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa
ya nyama eneo la Makunganya mkoani humo.
Naye
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu,
alieleza kuwa warsha hiyo iikuwa na manufaa makubwa na kwamba Wizara
inaandaa mkakati wa utekelezaji wa Sekta ya Fedha wa Miaka kumi ambao
utakujumuisha pia mawazo ya wadau hao.
Kwa
upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Honest Ngowi,
amepongeza hatua ya Serikali ya kuwa na majadiliano na Sekta ya fedha
kwa kuwa ina mchango mkubwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.
Akitoa
tathimini yake kuhusu utekelezaji wa Mpango huo, Prof. Ngowi, alisema
kuwa sehemu ya miradi kumi ya kipaumbele, ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati
kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ufufuaji wa Shirika la Ndege na Ujenzi
wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi mkoani Morogoro, ni baadhi ya miradi
muhimu inayotekelezwa.
Kwa
Upande wao, Mbunge wa Muheza Mhe. Adadi Rajab na Mbunge wa Viti Maalum
Mhe. Maria Kangoye, wamezishauri Sekta za Fedha nchini kuiwezesha zaidi
sekta ya kilimo ili ikue haraka na kuishauri pia Wizara ya Fedha na
Mipango, kufanya mikutano ya namna hiyo na wadau kabla ya Bunge la
Bajeti kuanza ii manufaa yake yaweze kuwa makubwa zaidi.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akifunga warsha ya
wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo
katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akizungumza
wakati wa kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga
kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo
Jijini Dodoma.
Mbunge
wa Jango’mbe Mhe. Ally Hassan King akizungumza wakati wa kufunga
warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta
hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Honest Ngowi akiongoza mjadala wakati wa
warsha ya wadau wa sekta ya fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta
hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
Mmoja
wa wadau wa Sekta ya Fedha akizungumzia umuhimu wa ushirikishwaji wa
sekta hiyo katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo hapa nchini
ili kuchochea maendeleo.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Dkt. Boghayo
Saqware akizungumzia hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wajumbe wa
warsha ya wadau wa sekta ya fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta
hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments:
Post a Comment