Mwenyekiti
wa halmashauri ya Mkuranga ,Juma Abeid akizungumza jambo katika kikao
cha baraza la madiwani ,wa kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo
,Mshamu Munde.
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
MWENYEKITI
wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkuranga, Filberto Sanga,
ametoa tathmini ya awali ya maafa yaliyotokea katika mvua zilizonyesha
hivi karibuni ambapo wanafunzi watano wamepoteza maisha kwenye mvua
hizo. Aidha ametoa tahadhari kwa watu na watoto kuacha kukatiza katika
mito na maeneo hatarishi ili kuepukana na maafa yanayoweza kujitokeza.
Akitoa
tathmini hiyo kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, Sanga alitaja
kata walizopoteza watoto hao kuwa ni Tambani wanafunzi wawili ambao
walizama, kata ya Mianzi, Mwarusembe,Mwandege mwanafunzi mmoja mmoja.
Alieleza kuwa, pia ipo miundombinu ya barabara ambayo imeharibika vibaya
na haipitiki. Sanga alisema ,wakati mvua ikiwa ni neema lakini
mazingira yalishindwa kuhimili ,hivyo wamejipanga kuanza kukarabati
baadhi ya miundombinu baada ya mvua kukoma. Alifafanua ,tathmini bado
inaendelea na watatoa ukubwa wa maafa yaliyotokea baadae.
Diwani viti maalum Mkuranga, Daima Utanga akizungumza jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani wilayani humo .
WAKATI
HUO HUO , Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga
wamemtaka afisa elimu msingi wa halmashauri hiyo, kuweka wazi idadi ya
shule zilizotumika kiasi cha fedha mil.29. Fedha hizo ni kati ya mil.151
iliyopangwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa shule mbalimbali
wilayani humo ambapo inadaiwa kutumika mil.29 .
Diwani
wa kata ya Mwandege ,Kowero Edward na diwani wa viti maalum Daima
Utanga waliibua hoja hiyo, katika kikao cha madiwani kilichofanyika
wilayani hapo. Walitaka kujua zilizotumika kwenye ukarabati na ujenzi wa
madarasa na shule ngapi kwani taarifa inaonyesha gharama bila idadi ya
shule husika, zilizotumika fedha hiyo.
"Tunahitaji majibu ya fedha hizi ,na mchanganuo ili tuweze kujiridhisha" alieleza Daima.
Nae
Mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji ,Shaban Manda alibainisha
,fedha hizo zimetumika kweli lakini kutokana na suala la idadi ya shule
zilipoelekezwa fedha hizo ,watarejea kwenye kamati na kikao kijacho
kutaletwa majibu ya uhakika ya hoja hiyo.
Alisema
,afisa elimu msingi wa halmashauri ya Mkuranga ni mgeni ,hivyo kutokana
na hilo ,hawezi kuwa na majibu ya moja kwa moja. Manda ,alieleza jumla
ya Tsh. mil.151 zimetengwa kwa ajili ya kukarabati na ujenzi ambapo hadi
sasa mil.29 pekee.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,Juma Abeid alisema masuala
ya fedha na matumizi yazingatiwe ili kuondoa maswali kwa madiwani.
Alisema ,uongozi wowote ni vijiti hivyo hakuna ugeni kwenye ofisi. Abeid
aliwataka madiwani wawe na subira ,kuiachia kamati kwenda kukaa ,na
kikao kinachofuata watapatiwa majibu ya uhakika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde alisema wanajivunia kupata hati safi .
"Hati safi hii tuliyoipata sio sifa ya mtu mmoja ,tunajipongeza wote watendaji,mbunge wetu Abdallah Ulega, madiwani na wilaya ";
",Tusiishie
hapa tuendelee na jitihada na kufanya kazi kwa kujituma ili kwenda na
kasi ya serikali ya awamu ya tano" alifafanua Munde.
Aliwaomba
watendaji kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya wanaMkuranga. Munde
alisema ,ushirikiano ndio nguzo pekee katika utendaji kazi hivyo
aliwaomba watendaji hao na madiwani kuwa kitu kimoja ili kuleta
maendeleo chanja na kuinua uchumi.
No comments:
Post a Comment