Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao
cha Baraza la Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara
ya kwanza katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la
Kwehangara.
Alisema iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo
inatoa mwanya kwa wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango
vinavyotakiwa hali inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha
zinazotumika.
“Ndugu zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya
maendeleo hili ndio jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo
wakandarasi wanafanya miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake
gharama inayotumika inakosa thamani yake”Alisema DC Lugangika.
Aidha pia alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Peter
Nyalali kuweka utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi
inayotekelezwa hususani miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa
kutokana na wakandarasi”Alisema
Nay kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli
Amiri Sheiza alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwasaidia
kuwatatulia mambo mawili makubwa kwao kuyapatia ufumbuzi.
Alisema suala la kwanza ni ujenzi wa Jengo la Halmashauri
eneo la Kwehangara na pili ni ufunguzi wa kiwanda cha Mponde katika
mambo hayo ameonyesha namna anavyotujali.
“Hivyo tunamuomba Mungu amuongezee hekima na busara katika
kuiendesha nchi na pia napenda kumthibitishia Rais kwamba wananchi,
Baraza la Madiwani pamoja na kupishana kifikra bado tupo pamoja kufanya
kazi bila kubaguana”Alisema.
Hata hivyo alionya kuwa mtu ambaye ataanzisha vimaneno
kuhusu suala hilo watamchukulia hatua kali kwa sababu atakuwa hana nia
njema na wananchi wa halmashauri hiyo katika kuwaletea maendeleo.
“Nionyesha mtu yoyote atakayeleta vimaneno kuhusu suala
hili sisi hatutamvumilia tutamchukulia hatua kali kwani wana Bumbuli na
mbunge wetu sote pamoja “Alisema.
(Habari kwa hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha)
Oscar Assenga
assengaoscar@gmail.com

إرسال تعليق