NA TIGANYA VINCENT
HATIMAYE
wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) mkoani Tabora
kwa kauli moja wameridhia kuganishwa kwa Chama Kikuu cha Ushirika kwa
ajili ya kuchukua Wilaya za Urambo na Kaliua ili kuanzisha chama kingine
kipya cha maeneo hayo.
Hatua
hiyo imefikiwa na viongozi kutoka Vyama vya Msingi (AMCOS)mbalimbali
kwenye Mkutano Mkuu wa 25 ulifanyika jana mjini Tabora.
Kaimu
Mrajis Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule alisema
uamuzi wa kuchukua baadhi ya wanachama wa WETCU na kuanzisha Chama kipya
ni kurahisisha usimamizi wa vyama vya msingi na kutekeleza agizo Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuvunja Bodi ya WETCU kwa sababu ya
kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za
umma.
Alisema
kuwa WETCU itaendelea kubaki na usajili wake wa awali na itakuwa na
Vyama vya Msingi(AMCOS) kutoka Uyui, Tabora Manispaa, Nzega na Sikonge.
Haule
aliongeza kuwa kisheria kama Chama cha WETCU kingevunja ingechukua hata
miaka miwili kuanzisha kingine na baada ya kufanyika ufilisi na ndipo
chama kipya kianzishe , ndio maana wameona ni vema kiendelee na usajili
ule ule na kianzishwe kipya kitakacho hudumia Urambo na Kaliua.
Alisema
kuhusu madeni yatabaki Chama cha WETCU na kile kipya cha
kitakachoanzishwa kitaanza bila deni kama takwa la kisheria
linavyohitaji ili kiwe na sifa ya kusajiliwa.
Haule
alisema viongozi wanaweza kukutana na kupendekeza jina la Chama kipya
au kinaweza kuitwa UKACU ili kuendelea na taratibu za usajili na kuahidi
kutangaza Bodi ya Mpito wa Chama kipya tarajiwa hivi karibuni ili
hatimaye ifikapo tarehe 16 Mwezi ujao(Juni) kiwe kimesajiliwa.
Alisema
baada ya usajili wanaweza kuitisha Mkutano wa uchaguzi kwa ajili ya
kuwapata viongozi wao ili waweze kuwahi msimu wa mauzo ya tumbaku
ulizindiliwa juzi wilayani Kahama.
Mmoja
wa wakulima ambaye pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo
Adamu Malunkwi alipongeza mapendekezo ya Serikali ya kupunguza ukubwa
na WETCU kwa kuwa ndio ulikuwa kisababisha ubadhirifu kwa sababu ya
viongozi kuwa na eneo kuwa na hivyo kushindwa kuvisimamia vema vyama vya
msingi.
Alisema
kuwa chama kitakachoanzishwa kitakuwa karibu na Vyama vya Msingi na
hivyo kuwaondoa wakulima katika mateso na kukosa tija kwa sababu ya
usimamizi mbovu unaotokana na ukubwa.
Mapema
mwaka jana (Machi 16, 2017) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliagiza
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora kuwakamata viongozi wanne wa Chama
Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha
za chama hicho.
Pia
baada ya kuvunja Bodi ya WETCU alipendekeza igawanywe na iwe na vyama
viwili vikuu kwa ajili kuwa Chama Kikuu cha Ushirika kitakachoweza
kuzisimamia vizuri AMCOS kwa ajili ya manufaa ya mkulima.
Kaimu
Mrajis Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule aakitoa
ufafanuzi ya taratibu za ugawaji wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku
(WETCU) na kuanzisha Chama kipya kwa ajili Wilaya za Urambo na Kaliua
jana mjini Tabora wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa chama hicho.
Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Nathalis Linuma alitoa maoni yake jana
wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku
(WETCU) ulifanyika mjini Tabora.
Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Tumbuku Hassan Wakasubi
alitoa maoni yake jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha
Ushirika wa Tumbaku (WETCU) ulifanyika mjini Tabora.
Baadhi
ya Viongozi wa Vyama vya Msingi (AMCOS) wakifuatilia mada mbalimbali
jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku
(WETCU) ulifanyika mjini Tabora.
No comments:
Post a Comment