Imeelezwa
kuwa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa fursa kubwa za maendeleo ya
kiuchumi na biashara kuliko nchi nyingine zote za Afrika Mashariki, na
kutolea tuu mfano wa sekta moja ya usafiri na usafirishaji, Tanzania
imeelezwa kuwa ni nchi yenye bahati sana, kuzungukwa na nchi 8 ambazo
hazina bahari, hivyo fursa tuu za usafirishaji kwa kutumia bandari,
reli, maziwa na anga, zikitumiwa vizuri, zinaweza kuipaisha Tanzania
kiuchumi na kujiendesha, bila kutegemea sekta nyingine zozote.
Bahati
hiyo imeelezwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa,
Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati wa hafla ya utiaji saini
mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na
Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor
Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia
Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.
John
Ulanga, amesema Tanzania imepakana na nchi nyingi ambazo hazina bahari
kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika Mashariki, hivyo Tanzania
ikichangamkia kutumia fursa hii kibiashara, itakuza uchumia sio tuu wa
Tanzania pekee, bali hata wan chi za jirani zetu, na kule kote njia hizi
zinakupita, maeneo hayo yana fursa za kustawi kiuchumi.
Ulanga
amesema, Tanzania imekana na nchi nane ambazo hazina bahari, nchi hizo
ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidekrasia ya Kongo, Zambia,
Malawi na Msumbiji, na kusema kama tutazizatiti na kusafirisha mizigo
yote ya nchi hizi, pato la usafirishaji pekee litakuwa kubwa kuweza
kuendesha nchi, hata bila kutegemea sekta nyingine.
Kwa
upande wake, Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne
Dukundane, ameishukuru TradeMark kwa ufadhili huo na kueleza fedha hizo
zitasaidia sana katika kutimiza majukumu ya CCTTFA ikiwemo uhamasishaji
wa matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuelezea faida za Bandari ya
Dar es Salaam ukilinganisha na bandari nyingine.
Naibu
Mkurugenzi wa Trademark East Africa, Bi. Monica Hangi amesema, kwa
vile lengo la Trademark ni kusaidia kurahisisha biashara, hivyo ufadhili
huo utasaidia sana kurahisisha biashara ya usafirishaji watu na mizigo
kwa nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.
Mkurugenzi
wa Miundombini wa TradeMark East Africa, tawi la Tanzania, Smark
Kaombwe, amesema biashara ni ushindani, hivyo ili bandari ya Dar es
Salaam iweze kuvutia zaidi nchi majirani waitumie, lazima iboreshe
utendaji wake mizigo ichukue muda mfupi kutoka, na pia iwe na gharama
nafuu kuliko bandari majirani zetu.
Meneja
Mradi wa Uangalizi wa Usafirishaji wa Central Corridor, Eng. Melchior
Balentandikye, amesema kabla ya msaada huo, Central Corridor imekuwa
ikijihusisha na usafiri wa barabara pekee, lakini sasa msaada huo,
utawasaidia kushughulikia usafiri wa barabara, reli na usafiri wa majini
na usafiri wa anga.
Meneja
wa Fedha na Utawala wa Central Corridor, Costaph Natay, amesema msaada
huo utasaidia sana kuboresha ufanisi, hivyo Central Corridor itaboresha
ufanisi wa shughuli zake, hivyo kuongeza ufanisi katika usafirisha
abiria na mizigo katika ukanda wa kati.
Meneja
Mawasiliano wa Central Corridor, Flory Okadju, amesema msaada huo
utaisaidia Central Corridor kuboresha mawasiliano na utoaji wa elimu kwa
umma katika nchi zote tano za Ukanda wa kati, hivyo kutoa uelewa mkubwa
zaidi kuhusu ubora na unafuu wa bandari ya Dar es Salaam, hivyo kuvutia
zaidi wafanyabiashara wan chi hizi, kupitishia mizigo yao bandari ya
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John
Ulanga, akionyesha njia za Ukanda wa Kati, wakati wa hafla ya utiaji
saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni
karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central
Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo
inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda,
Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa
Kati.
Mkurugenzi
Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John
Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt.
Diodonne Dukundane wakitia saini mkataba, wakati wa hafla ya utiaji
saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni
karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central
Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo
inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda,
Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa
Kati.
Mkurugenzi
Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John
Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt.
Diodonne Dukundane wakibadilishana mkataba, wakati wa hafla ya utiaji
saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni
karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central
Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo
inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda,
Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa
Kati.
No comments:
Post a Comment