
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa maelezo
ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu kwa wakulima wa pamba katika
Wilaya ya Nzega. Mkuu wa Mkoa huyo alikuwa katika ziara maalumu ya
kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa mbalimbali katika mashamba ya
wakulima wa pamba katika sehemu mbalimbali Wilayani humo.
Mshauri
wa Masuala ya Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest
Kaijage (mwenye shati nyeupe) akitoa kwa wakulima namna ya kuwatambua
wadudu mbalimbali waharibifu wa zao la pamba katika Kijiji cha Mogwa
Wilayani Nzega wakati wa ziara maalumu ya Mkuu wa Mkoa huo kuhamasisha
matumizi sahihi ya dawa mbalimbali kuua wadudu katika mashamba ya
wakulima katika sehemu mbalimbali Wilayani Nzega.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa elimu
Wilayani Nzega juu ya matumizi ya dawa ya kuua wadudu waharibifu wa
pamba aina ya Dudu -All 450EC wakati wa mwendelezo wa kampeni yake ya
kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya viuawadudu.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia ) na Mkuu wa Wilaya ya Nzega
Godfrey Ngupula (kushoto) wakigagua shamba la Mkulima wa pamba katika
kijiji cha Chamwabo wilayani Nzega ambalo lilikuwa limeathiriwa na juu
na wadudu waharibifu lakini hivi limeanza kuanza matunda mapya ya
pamba(vitumba).
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) akitoa elimu kwa wakulima wa
pamba wa Kijiji cha Budushi wilayani Nzega juu ya matumizi sahihi ya
aina mbalimbali ya dawa za kuua wadudu wa zao la pamba. Wengine ni Afisa
Ugani Kata ya Kitangili Halima Chezue(wa pili kulia), Mtendaji wa
Kijiji cha Budushi Ndimiyake Noah (wa pili kutoka kushoto) na Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Kitangili Jesca Kaaya(kushoto)
Miongoni
pamba ambayo imetunzwa vizuri na kupuliziwa dawa vizuri ya kuua wadudu
waharibifu katika shamba la Mkulima wa Kijiji cha Budushi Christina
Bundala kama inavyoonekana.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) akimpongeza Mkulima wa Kijiji
cha Budushi Wilayani Nzega Christina Bundala (kushoto) kwa kutunza
vizuri shamba lake la pamba na kuweka vitumba vingi vya pamba(matunda)
wakati akiwa ziara yake ya kuendesha kampeni ya utunzaji vizuri wa
mashamba ya pamba kwa kupulizia sahihi dawa za kuua wadudu waharibifu.
Baadhi
wa wakulima wa Kijiji cha Kitangili wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Mkoa
wa Tabora (hayupo katika picha) wakati akiwa ziara yake ya kuendesha
kampeni ya utunzaji vizuri wa mashamba ya pamba kwa kupulizia sahihi
dawa za kuua wadudu waharibifu.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiongea na waandishi wa habari kwenye
shamba la Mkulima Christina Bundala (hayupo katika picha)wa Kijiji cha
Budushi wilayani Nzega wakati akiwa ziara yake ya kuendesha kampeni ya
utunzaji vizuri wa mashamba ya pamba kwa kupulizia sahihi dawa za kuua
wadudu waharibifu.
Picha zote Tiganya Vincent










إرسال تعليق