Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi ametaja maboresho kadhaa yaliyofanyika katika Wizara ya Ardhi.
Mhe.
Lukuvi aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika
kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
Akieleza
Maendeleo yanayofanyika sasa katika eneo la Urasimishaji; Mhe Lukuvi
alieleza kuwa zoezi la Urasimishaji sasa linaendelea kwa kasi, na
kutolea mfano wa Jiji la Mwanza kuwa zoezi hilo linafanyika kwa
mafanikio makubwa. Alisema; “Mpaka sasa viwanja 35,000 vimeshapimwa na
Hati 12,000 kutolewa katika wilaya za Ilemela na Nyamagana.
Mhe.
Lukuvi alisema baadhi ya maeneo mengine ambayo yamefanya zoezi la
Urasimishaji kwa kiwango cha kuridhisha ni pamoja na Kimara na Makongo
ambapo Wananchi wenyewe wamekuwa wahusika wakuu katika kuhakikisha kuwa
wamezingatia miongozo waliopewa na Wizara kufanikisha zoezi hilo,
ikiwepo kuzingatia kuainisha miundombinu muhimu kama njia za barabara,
maji , umeme n.k.
Akiendelea
kufafanua jinsi eneo la Upimaji wa viwanja lilivyoboreshwa. Mhe. Waziri
ameeleza kuwa sasa kuna kampuni 48 za upimaji ambazo zimesajiliwa na
kuidhinishwa na Wizara, na zinazoendelea sasa na kufanya upimaji wa
viwanja katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha,
Mhe . Lukuvi ameeleza kuwa katika maeneo ya Vijijini pia kasi ya
upangaji wa Matumizi bora ya Ardhi imekuwa ya kuridhisha, tofauti na
miaka ya zamani. Hatahivyo alieleza kuwa changamoto zipo, hususani
katika mkoa wa Morogoro; katika maeneo ya Mvomero, Kilombero na
mengineyo lakini Serikali inaendelea na jitihada za kufanya taratibu za
upangaji wa Matumizi bora ya Ardhi na kufanya upimaji wa maeneo kwa kasi
kubwa zaidi katika maeneo hayo.
Vile
vile Mhe. Lukuvi amesema katika kuboresha ulinzi wa Hati za Ardhi; Hati
sasa zipo katika taratibu za kuandaliwa na kutolewa Kielektroniki.
Alisema, Hati hizo za Kielektroniki zitathibiti mianya yote ya ulaghai
na rushwa, matendo ambayo yamekuwa yakifanywa kwa muda mrefu na matapeli
mbalimbali na kusababisha vilio kwa Wananchi wengi. Pia kwa Mfumo huo
wa Kielektroniki kila Mmiliki wa Ardhi, atalazimika kuwajibika ipasavyo
katika kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.
Naye
Mzee Butiku amempongeza Mhe. Lukuvi katika juhudi zake za kuendelea
kuboresha huduma zinazofanywa na Wizara hiyo na kumsihi kuendelea na
jitihada hizo. Alisema; “Nikilinganisha hali iliyokuwepo Wizarani
nyakati za nyuma na sasa, maboresho ni makubwa, endelea na juhudi
unazozifanya”.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha
muonekano wa Hati ya Kielektroniki inavyotarajiwa kuwa kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere; Mzee Joseph Butiku alipofika
ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha
moja ya ramani za Mipango Miji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika
kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akiagana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku na
msaidizi wake walipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya
Ardhi - Dar es Salaam.

Post a Comment