Waziri
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
(katikati mbele) akiwa katika chumba cha mikutano cha Kampuni ya ujenzi
ya Kimataifa ya Uholanzi (BAM) linalojenga Jengo la tatu la abiria la
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII)
alipofanya ziara. (Wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na
(wa kulia) ni Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul.
Mkandarasi
wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere, Bw. Wolfgang Marschick (katikati kushoto) akitoa
maelezo ya ujenzi huo leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanza nia (TAA), Bw. Richard Mayongela.
Waziri
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof. Makame Mbarawa
(kushoto) akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela wakati
walipokuwa wakitembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII). Nyuma ni Kaimu
Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka.
Mkandarasi
wa mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Wolfgang Marschick
(Kulia) akimuonesha waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.
Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) leo alipotembelea jengo hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Bw. Richard Mayongela (katikati).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye
miwani mbele) akimsikiliza Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la
abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TBIII), Bw. Wolfgang Marschick (aliyenyoosha mkono) na wapili
kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Richard Mayongela.
Balozi
wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul akiongea na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof.Makame Mbarawa (wa tatu kulia)
alipofanya ziara ya kutembelea jengo hilo leo. Wengine katika picha ni
Bw. Wolfgang Marschick (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (pili kulia).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa
(aliyesimama mbele), leo akiongea na wadau wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), kwenye ukumbi wa Watu
Mashuhuri (VIP). Mbele kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.
WAZIRI
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka
wadau wanaofanya shughuli mbalimbali zinazohusisha na kodi ya pango
kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere (JNIA),
kuhakikisha ifikapo Februari 1, 2018 wawe wameshalipa madeni yao.
Prof.
Mbarawa alisema leo wakati alipoongea na wadau hao kwenye ukumbi wa watu
Mashuhuri wa JNIA-TBII, wakati walipozungumza nao kujadili masuala
mbalimbali.
Alisema
baadhi ya wadau wameshalipa madeni yao kati ya bil 10 zilizokuwa
zinadaiwa na sasa zimesalia bil. 3.7 ambapo amewataka baada ya
kumalizika kwa sherehe za Krismas na Mwaka Mpya wahakikishe
wanakamilisja madeni yao.
“Hatutasita
kumuondoa mtu yeyote atakayekuwa akiendelea kudaiwa kwani atakuwa hana
sifa za kupangisha katika majengo haya ya viwanja vya ndege kwa kuanzia
TBI na hapa TBII,” alisema Prof. Mbarawa.
Hatahivyo,
aliyapongeza mashirika na ofisi ambazo zimekuwa zikilipa kwa wakati
fedha za pango, ambapo uaminifu huo utawasaidia kupata nafasi katika
jengo jipya la la tatu la abiria, ambalo litakuwa linauwezo wa kuhudumia
abiria milioni sita (6) kwa mwaka.
Pia
amewataka wale wasiowaaminifu wachague kulipa madeni ya pango au
wanaodaiwa na serikali au kuondoka, ili kutoa nafasi kwa Watanzania
wengine ambao wanania ya dhati ya kufanya biashara na Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege Tanzania (TAA), wasimamizi wakuu wa viwanja vya serikali.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela alisema tayari zabuni
mbalimbali zimeshatangazwa na kuwataka wadau waliowaaminifu kujitokeza
kuwania na kupata nafasi ya kufanya shughuli zao kwenye eneo la JNIA.
“Tumeshatangaza
zabuni hizo na kama mhe. Waziri alivyosema zitakuwa za uwazi
zikishirikisha wataalamu na tunauhakika watapatikana watu wenye mapenzi
mema ya kufanya biashara na serikali” alisema Bw. Mayongela.
Katika
hatua nyingine, Prof. Mbarawa alitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la
tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TBIII) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi, ambapo amewapongeza TAA,
Tanroads na Kampuni ya ujenzi ya Kimataifa ya Uholanzi (BAM).
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Bw. Mayongela, alisema kukamilika kwa jengo
hilo kutatoa fursa nyingi za biashara zikiwemo uwekezaji katika hoteli,
kumbi za mikutano, ofisi, migahawa, maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali,
huduma za kifedha (benki) na karakana za ndege.


إرسال تعليق