Benki
ya TIB imetoa msaada wa vitanda viwili pamoja na mashine ya kupumulia
kwa mtoto mwenye tatizo la kupumua katika zahanati ya Msongola , Ilala
jijini Dar es Dar es Salaam.
Akizungumza
baada kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo amesema
kuwa benki inaguswa na afya za wananchi pamoja na watoto.
Amesema
kuwa benki itaendelea kutoa msaada mbalimbali kwa ajili ya wananchi
wake ambao ndio mtaji wa benki pale wanapopata huduma bora za afya.
Nae
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema msaada huo ni muhumu
katika zahanati ya Msongola na kuwata benki hiyo kuendelea kuunga mkono
zahanti katika kuweza kutoa huduma bora.
Amesema
serikali ina mambo mengi pale panapotokea wadau wanajitolea wanakuwa
wameisaidia serikali katika kutatua changamoto na kuweza kuendelea
kutoa huduma nyingine sehemu zenye changamoto.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo(kulia)
akimkabidhi vifaa vya matibabu Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema
kwa niaba ya Zahanati ya Msongola vyenye thamani ya shilingi milioni
saba (7) walizochanga wafanyakazi wa benki hiyo ili kusaidia wakina mama
wanaojifungua katika Zahanati hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Ukonga, Mwita
Waitara.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari,
wafanyakazi wa TIB Corporate Benki, Wauguzi na wananchi wa Msongola mara
baada ya TIB Corporate Benki kukabidihi msaada wa vifaa vya matibabu
kwenye Zahanati ya Msongola leo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu benki hiyo inavyorudisha fadhila kwa wananchi
kwa kusaidia kwenye masuala ya kijamii ikiwemo na msaada walioutoa
kwenye Zahanati ya Msongola.
Mganga
Mfawidhi wa Zahanati ya Msongola, Dk. Mwanahawa Malika akitoa shukrani
kwa TIB Corporate Benki kwa kusaidia zahanati hiyo
Baadhi vifaa vilivyotolewa na TIB Corporate Benki kwenye Zahanati ya Msongola leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa TIB Corporate Benki wakiwa kwenye picha ya pamoja

إرسال تعليق