Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya maji na Umwagiliaji Paul Suley aliyekuwa anamwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya maji na Umwagiliaji amesema kuwa amezipokea changamoto ya shule hiyo na atawasilisha wizarani kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Shule ya Msingi Tabata
ulioratibiwa na aliyekuwa Miss Ubungo 2014, Diana Kato uliogharimu
takribani shilingi 613,000 za kitanzania.
Sulley
alisema kuwa, amezipokea changamoto zao ikiwemo ya kutokuwa na tanki la
kuhifadhia maji ataliwasilisha wizarani na pia amefurahi sana kuona
wadau mbalimbali wanajitoa kwa ajili ya kusaidia jamii.
Diana
Kato amesema kuwa ameweza kutoa msaada huo kwa shule ya msingi Tabata
ikiwa ni katika moja ya mradi ambapo alitumia takribani kiasi cha
shilingi 613,000 kwa ajili ya kulipia gharama za kuwekwa maji na kununua
vifaa vya ujenzi ili kukamilisha mradi huo.
Miss
Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato akisoma risala kuhusu historia fupi
kuhusu alivyoanza kutekeleza mradi wa bomba la maji safi uliokamilika na
kukabidhiwa katika shule ya Msingi Tabata.
Mgeni
Rasmi Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Paul Sulley aliyekuwa anamwakilisha Katibu mkuu wa Wizara
hiyo akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi walioudhulia uzinduzi wa
bomba la maji safi katika shule ya Msingi Tabata iliyopo Ilala jijini
Dar es Salaam . Kushoto ni alifadhiri mradi huo Miss Ubungo 2014,
Diana Joachimu Kato na kulia ni Mkuu wa Shule ya msingi Tabata, Hamisi
Ngoda.
Mkuu
wa Shule ya msingi Tabata, Hamisi Ngoda akizungumza na wazazi pamoja na
wanafunzi wakati wa uzinduzi wa bomba la maji kwenye shule hiyo
lililofadhiliwa na aliyekuwa Miss Ubungo Diana Kato leo shuleni hapo.
Wanafunzi wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa bomba la maji safi lililofadhiliwa na aliekuwa Miss Ubungo 2014.
Baadhi
ya wazazi na wanafunzi wakufuatilia tukio la kukabidhi Bomba la maji
kwenye shule ya Msingi ya Tabata, Ilaa jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya Maji na Umwagiliaji, Paul
Sulley akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bomba la maji kwa ajili ya
matuminzi mbalimbali katika shule ya Msingi Tabata jijini Dar es
Salaam.
Picha pamoja mara baada ya kuzindua bomba la maji safi kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni hapo.

إرسال تعليق