Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametembelea vituo sita vya
huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na
Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga yenye vituo tisa.
Mkuu
huyo wa wilaya amefanya ziara hiyo leo Jumamosi Disemba 2,2017 kwa ajili
ya kujionea stadi za maisha na miradi mbalimbali inayofanywa na watoto
wanaopata huduma katika vituo hivyo.Vituo
vilivyotembelewa ni vituo vya Kanisa la ACT Shinyanga Mjini,AICT
Kolandoto,TAG Shinyanga Mjini,PAG Shinyanga Mjini,KKKT Shinyanga Mjini.
Akiwa
katika ziara hiyo,Matiro amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na
watoto kama vile utengenezaji skonzi,biskuti,keki,nguo,mafuta,sabuni
pamoja na ususi,ufumaji,saluni,ufyatuaji wa matofali,uchomeleaji wa
vyuma,useremala,masomo ya kompyuta na mambo mengine kadha wa kadha.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo,mkuu huyo wa wilaya alilipongeza shirika la
Compassion kupitia makanisa yanayosimamia vituo hivyo ambavyo vimekuwa
msaada mkubwa kwa watoto ambao wanajengewa uwezo wa kujiajiri.
“Nimegundua
tuna jeshi kubwa la vijana wenye ujuzi wa aina mbalimbali,vijana
tumieni fursa hii ya Compassion kujinufaisha kwa ajili ya maisha
yenu,sisi kama serikali tunafarijika sana kuona vijana wakijengewa uwezo
wa kujiajiri ili kuleta maendeleo katika jamii”,alieleza. Matiro
alieleza kufurahishwa kuona jinsi vijana hao wanavyojengewa uwezo wa
kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwashauri kuongeza jitihada ili
kutengeneza viwanda kamili vya kutengeneza bidhaa.
“Sera
ya serikali ni kuwa na viwanda,nimeona vijana wanatengeneza
skonzi,biskuti kwa kutumia mashine za kisasa kabisa katika kituo cha
AICT Ngokolo,hiki ni kiwanda,naomba kanisa na Compassion kwa
kushirikiana na serikali tuangalie namna ya kupanua kiwanda hiki ili
kuleta mabadiliko katika jamii na kitasaidia vijana kujikwamua
kiuchumi”,alisema Matiro.
Katika
hatua nyingine aliwataka wahusika katika vituo hivyo kuhakikisha msaada
unaotolewa na shirika hilo kuwafikia watoto wanaolengwa huku akiwataka
kushirikiana kwa ukaribu na viongozi wa serikaliza mitaa ili kubaini
watoto wanaohitaji msaada kutokana na ugumu wa maisha.
Awali
akisoma taarifa kuhusu vituo vya huduma ya mtoto katika klasta ya
Shinyanga,Katibu wa wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Thomas Faida
alisema shirika la Compassion linahudumia watoto 2,110 wanaoishi kwenye
mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga. Alisema
watoto hao hupatiwa misaada mbalimbali kama vile kufundishwa stadi za
maisha,kupewa elimu ya ujasiriamali,kupewa sare za
shule,madaftari,nguo,ada ya shule,gharama za matibabu na mambo mengine
kadhaa.
Kwa
upande wake Msimamizi wa vituo vya huduma ya mtoto klasta ya Kanda ya
ziwa,Emmanuel Pando alisema shirika la Compassion linafanya shughuli
zake kwa ushirika wenza na makanisa katika kuwahudumia watoto walioko
katika mazingira magumu.
Pando
alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ili
kufanikisha mambo mbalimbali ambayo serikali inataka yafanikiwe.
Mwenyekiti
wa Wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa
la TAG Shinyanga akimpokea mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini kwa ajili ya kutembelea
stadi za maisha na miradi inayofanywa na watoto katika kituo hicho.
Mkurugenzi
wa kituo cha huduma ya watoto kanisa la ACT Shinyanga Mjini,Hagai
Daniel akimwongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwenda kuangalia stadi za
maisha na miradi inayofanywa na watoto wanaohudumiwa katika kituo
hicho.
Vijana
wakimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro keki
walizotengeneza.Vijana hao walisema wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza keki
katika kituo hicho.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi
wanavyochomelea vyuma katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba cha ufumaji katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba kwa ajili ya mambo ya ususi.Vijana wanaendelea kusukana.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipokelewa katika kituo cha
Kanisa la AICT Kolandoto. Wa kwanza kulia ni diwani wa kata ya
Kolandoto,Agnes Machiya,ambaye ni pia ni naibu meya wa manispaa ya
Shinyanga.Katikati ni Mchungaji Kiongozi kanisa la AICT Kolandoto,Jacob
Osora
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika chumba cha
Kompyuta katika kituo cha AICT Kolandoto.Kulia ni mwalimu wa Kompyuta
katika kituo hicho, Lucas Masaba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha AICT Kolandoto.
Watoto katika kituo cha AICT Kolandoto wakiimba wimbo
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi watoto
wanavyotumia kompyuta katika chumba cha kujifunzia Kompyuta katika kituo
cha AICT Ngokolo.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimwangilia kijana akishona
nguo kwa kutumia cherehani katika kituo cha AICT Ngokolo
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia mashine zinazotumika
kutengeneza skonzi na biskuti katika kituo cha AICT Ngokolo. Mkuu huyo
wa wilaya alisema hicho ni kiwanda hivyo kinachotakiwa ni kuangalia
namna ya kukipanua ili kilete maendeleo.
Mmoja
wa vijana wanaotekeleza mradi wa kutengeneza skonzi na biskuti katika
kituo cha AICT Ngokolo akionesha moja ya mitambo waliyonayo katika kituo
hicho.
Kijana
James Emmanuel akionesha mtambo wa kupasulia mbao katika kituo cha AICT
Ngokolo.Alisema huwa wanatengeneza samani mbalimbali kama vile
stuli,viti na vitanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimia watoto katika kanisa la AICT Ngokolo
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa amevaa mkoba
uliotengenezwa kwa vitambaa laini katika kituo cha kanisa la TAG
Shinyanga Mjini.
Kijana
Rebeca Jeremiah akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro,moja ya vitambaa laini kwa ajili ya wanawake kujistiri wakiwa
katika hedhi 'Pad' ambazo amekuwa akizitengeneza na kuziuza.Rebeca
alisema pedi hizo unaweza kuzifua
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia pedi ambayo unaweza kuifua na kuitumia mara nyingi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpongeza Rebeca kwa ubunifu wa kutengeneza pedi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiwa katika kanisa la PAG Kambarage wakisalimiana na watoto
Kulia ni watoto wakiwa katika kanisa la PAG Kambarage
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa mbalimbali
zinazotengezwa na watoto katika kituo cha kanisa la KKKT Shinyanga
mjini.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kutoka kwa
watoto kuhusu namna wanavyotengeneza sabuni kwa ajili ya matumizi
mbalimbali ya nyumbani na ofisini.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati akiangalia
mitambo ya umeme iliyotengenezwa na watoto katika kituo cha KKKT
Shinyanga mjini
Hapa
ni katika ukumbi wa kanisa la KKKT usharika wa Ebenezer kanisa kuu
Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria: Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wa kikao cha majumuisho ya ziara
yake kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili
yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya
Shinyanga.
.
Katibu
wa wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Thomas Faida akizungumza
katika kikao cha majumuisho ya ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya
kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa
ya Shinyanga.
Msimamizi wa vituo vya huduma ya mtoto klasta ya Kanda ya ziwa,Emmanuel Pando akizungumza katika kikao hicho.
Katibu
Mkuu wa kanisa la KKKT usharika wa Ebenezer kanisa kuu Dayosisi ya
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Happiness Gefi akizungumza wakati wa
kikao cha majumuisho ya ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro kutembelea vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili
yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya
Shinyanga.
Mwenyekiti
wa Wachungaji klasta ya Shinyanga,Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa
la TAG Shinyanga akizungumza wakati wa kikao cha kikao cha majumuisho
ya ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kutembelea
vituo vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika
na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog



إرسال تعليق