Na David John Misungwi
WANANCHI
wa Kijiji cha Mwasonge kilichopo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza
wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa Daraja linalotenganisha wilaya
hiyo na Wilaya ya Nyamagana.
Wamesema
kuwa wananchi wa wilaya hizo hususani wanaoishi mpakani wamekuwa
wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na serikali kushindwa kujenga
Daraja.
Akizungumza
Wilayani hapa leo Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Mwasonge Masumbuko
Reuben alisema Tangu dunia iumbwe Serikali licha ya kutambua umuhimu wa
eneo hilo lakini haijawahi kutengeneza Barabara hiyo wala Daraja.
"Naiomba
sana Serikali yangu ifike mahala waone huruma dhidi ya wananchi hawa
ambao wengi wao wanakatisha hapa kwenda Buhongwa katika wilaya ya
Nyamaga kilometa mbili kuliko kuzunguka Usagala ambako ni zaidi ya
kilometa 10."amesema Masumbuko.
Ameongeza
kuwa eneo hilo linakuwa hatari zaidi linapojaaa maji kutokana na Mvua
ambazo wakati mwingine zinanyesha mfululizo na kusababisha kutumia
mitumbwi kuvusha wananchi hali inayohatarisha usalama.
Amefafanua
kuwa miaka ya hivi karibuni kutokana na eneo hilo kujaa maji
pameshawahi kutokea maafa ya raia hivyo kuna kilasababu na haja ya
serikali kujenga Daraja katika eneo hilo.
"kimsingi
tumesikia tu kwamba kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya eneo hili
lakini hadi leo hatuoni kitu chochote kinachoendela na tuna Muomba
Mbunge kufuatilia na kutusemea ili sisi wananchi wake tujengewe Daraja
hili. Amesema Masumbuko.
Akitolea
ufafanuzi juu ya eneo hilo linalolalamikiwa na wananchi Mbunge wa Jimbo
la Misungwi Charles Kitwanga amesema ni kweli fedha za ujenzi wa Daraja
hilo zipo kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni mia tisa.
"fedha
zipo kwani zilishatolewa na Tanroads na kilichobaki nadhani ni ujenzi
tu japo nimesikia tu kuna namna namna zinataka kufanyika mara upembuzi
lakini mimi ninachojuwa upembuzi yakinifu ulishafanyika na fedha za
ujenzi tayari. "amesema Kitwanga
Aidha
amesema yeye kama mbunge amelipigia kelele sana eneo hilo na nikweli
kwamba ni linaumuhimu kwa wananchi hao pande zote mbili kwa maana wilaya
ya Misungwi na wilaya ya Nyamagana.
Ameongeza
kuwa kutoka Mwasonge kwenda Buhongwa ni karibu zaidi kwa kukatiza eneo
hilo kuliko kuzungukia Usagala ambako kuna zaidi ya kilometa kumi.
"Naomba
Halmashauri ya Wilaya kama fedha hizi zimeshaingia na mimi najuwa hivyo
kuna haja ya kuaza ujenzi na nadhani hili ni kwa wilaya zote mbili kwa
maana ya Misungwi na Nyamagana. Amesisitiza Kitwangwa.


إرسال تعليق