Waziri
Mpina na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bukoba wakielekea katika zoezi
la upigaji chapa ng’ombe katika kata ya katerero kijijini Kyerwa leo.
Katika picha ikionekana sehemu ya ng’ombe aliyepigwa chapa katika kata ya Katerero kijijini Kyerwa leo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi.
Saada Malunde baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu
ya pori la Bugiri Biharamuro, wengine katika picha ni askari wanyamapori
wa pori hilo.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi
Saada Malunde wakizungumza baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo
katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro.
NA MWANDISHI MAALUM – KAGERA
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhanga Mpina amewataka wafugaji nchini
kutembea kifua mbele kwa kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya
Mifugo, Mpina ameyasema hayo leo aliposhiriki katika zoezi la kupiga
chapa Mifugo katika Kijiji cha Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero
halimashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera, na kuwataka viongozi
kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka
hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.
Waziri
Mpina alipofika katika kata ya Katerero aliwakuta wafugaji wamejitokeza
kwa wingi kuunga mkono zoezi la uwekaji alama katika mifugo yao na
kushiriki zoezi hilo kwa kuonyesha msisitizo.
Mara
Baada ya kushiriki zoezi hilo, Waziri Mpina aliwataka wafugaji hao
kuendelea kujitokeza kwa wingi na kuleta mifugo yao kupigwa chapa na
kusema kuwa zoezi hilo ni la manufaa na faida kwa wafugaji kwani
litaweza kuwasiadia kuhepuka maambukizi ya magonjwa ya wanyama kwa
mifugo yao kuto kuchanganyikana na mifugo mingine sambamba na kusaidia
upotevu wa mifugo.
Akiongea
katika zoezi hilo diwani wa kata ya Katerero Bw. Nuru Abdul Kabendera
alisema kuwa, amefurahishwa na ziara ya Waziri Mpina katika kata ya
katerero kwani ni mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka
katika ngazi ya juu ya serikali na kumuomba Mpina kupitia Wizara yake
kutatua changamoto inayoikabili kata hiyo la josho la kuoshea ng’ombe
ambapo Waziri Mpina amehaidi kuitatua.
Katika
hatua nyingine Waziri Mpina ametembelea mapori ya Burigi yaliyopo
wilayani Biharamulo ambapo ameupongeza uongozi wa mkoa kwa uporasheni
iliyofanyika ya kuondoa mifugo katika mapori tengefu na hifadhi za
misitu ambapo amewashuhudia wanyama pori ambao tayari wamerejea katika
mapori hayo huku mkuu wa wilaya hiyo Bi SAADA MALUNDE Akiwataka wananchi
wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano katika zoezi la kuondoa mifugo.
Aidha,
Mpina amewataka wakuu wa Mikoa ya mipakani kuwasilisha kwake taarifa ya
uondoshwaji wa mifugo katika mikoa yao mara baada ya kukamilika kwa
zoezi hilo la oparesheni ondoa mifugo.
Waziri
MPINA amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani kagera kubwa akiwa
ameagiza mifugo yote iliyokamatwa kutoka nje ya nchi itaifishwe na
kupigwa mnada haraka sana kwa mujibu wa sheria.


Post a Comment