Afisa kilimo Mkoa wa Mbeya (kulia) akipokea maelezo ya kilimo cha mbogamboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na TAHA katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Afisa Kilimo na Msimamizi wa ofisi ya TAHA ukanda wa Nyanda za Juu Kusini Bw. Ringo (Mwenye Jaketi jekundu) akifafanua juu ya matumizi bora ya teknoloji za kisasa kwenye kilimo cha mboga ili kuongeza tija kwa Mkulima katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Mtaalamu wa Kilimo wa TAHA Bw. Anania Bansimbile akiwaonyesha wananchi namna bora ya kuotesha mimea ya mboga kabla ya kupandwa shambani katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Karoti iliyovunwa kutoka katika vitalu vya TAHA kwa ajili ya maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nanenane Mbeya
Wananchi wakipewa elimu lishe kuhusu umuhimu wa matumizi ya mboga kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi. Lawrencia wakati wa maonyesho ya Nanenane Mbeya
No comments:
Post a Comment