Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe
akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti
Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti
Tengeru).
Baadhi
ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha
Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akiwasili
katika Ofisi za Taasisi ya Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga
Matunda na Maua (Horti Tengeru). Mwingine ni
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Taasisi ya
Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti
Tengeru).
Baadhi
ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha
Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Afisa Mfawidhi -Horti-Tengeru akisoma Risala kwa niaba ya watumishi wenzanke wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Baadhi
ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha
Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Bi Alice M. Kavishe akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Dkt Stephen Sebastian Kuoko akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe
akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti
Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti
Tengeru).
Baadhi
ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha
Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi.
Na Mathias Canal, Arusha
Serikali
imekuwa ikiongeza idadi ya wanafunzi katika Vyuo vya Kilimo na kwa
sababu hiyo Maafisa Ugani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka ambapo hali
hiyo imewezesha Karibu kila Kata hapa nchini kuwa na Afisa Ugani.
Lakini
pamoja na kuwepo kwa wataalamu hao wa kilimo bado uzalishaji wa mazao
mbalimbali nchini yakiwemo mazao ya chakula na biashara si wa kuridhisha
ambapo wakulima wanalima na kupanda pasina hata kufuata hatua za
kitaalamu.
Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew
John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi akizungumza na wakufunzi wa Chuo
cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI TENGERU) kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Alisema lengo la Serikali kusambaza Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ilikuwa kuwasaidia wakulima waweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi na kuongeza mavuno.
Hata
hivyo jambo hilo limekuwa kinyume kwani asilimia kubwa ya maafisa ugani
ama hawafanyi kazi zao ipasavyo ama wameshindwa kusimamia majukumu yao
ipasavyo.
Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Wizara ya kilimo inaandaa utaratibu wa kuwarudisha shule maafisa ugani wasiofaa
kutokana na uchache wa ellimu zao na uwajibikaji huku wale ambao
watashindwa kabisa kuwa msaada kwa wakulima baada ya masomo wizara
itapendekeza waondolewe kazini.
Alisema
Maafisa ugani hao Watafanyiwa usaili upya ili kubaini uwezo wao kwani
wengi wao wameajiriwa na serikali lakini wakulima hawanufaiki na kilimo
tafsiri yake Wataalamu hao ama hawatekelezi wajibu wao au hawana uwezo
wa kutekeleza ipasavyo.
Aidha, alisema Maafisa ugani kote nchini wanatakiwa kuwekeza
kwenye utoaji wa Huduma ya Ugani kwa Wakulima ili iwe rahisi kwa
Mkulima kusaidika katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ya biashara na
kilimo.
Sambamba
na hayo pia aliwasihi Wakufunzi katika chuo hicho kujiendeleza kielimu
huku akisema kuwa Wizara ya kilimo lazima itengeneze mpango wa
kuwaendeleza wakufunzi ili kuzalisha wataalamu wenye ufanisi zaidi.
Alisema
anatambua kuwa Mahitaji ni makubwa katika vyuo vya kilimo hivyo Wizara
inatazama namna ya kuongeza chuo kingine kama hicho huku akiwasisitiza
wataalamu hao kubadili mfumo badala ya kusoma kwa jumla masomo mengi na
kufikia hatua ya kuchagua eneo maalumu la kusoma (Kozi) kwani Kilimo ni
somo pana.
“Nategemea
muandae mpango maalumu ambao utapelekea Kuwa na kozi za muda mchache
sio lazima kuwa na kozi za muda mrefu pekee kama ilivyo hivi sasa”
Alisema Mhandisi Mtigumwe
Katika
hatua nyingine amewataka Watumishi wote kuongeza spidi katika utendaji
wa kazi ili kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali ya awamu ya tano yenye
kauli mbiu ya HapaKaziTu.
Sambamba
na kutembelea na kuzungumza na watumishi na wakufunzi wa Chuo cha
Mafunzo ya Mbogamatunda na Maua (HORTI TENGERU) Akiwa ziarani Mkoani
Arusha Katibu Mkuu Mhandisi Methew Mtigumwe alitembelea pia Taasisi ya
Utafiti Horti Tengeru, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda
ya Kaskazini (NZARDI) na Taasisi ya Utafiti ya kudhibiti visumbufu
katika Ukanda wa Tropiki.








Post a Comment