Shule
ya Sekondari Kom iliyopo mjini Shinyanga Jumamosi Novemba 11,2017
imefanya mahafali ya 9 ya kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo
mwaka 2006.
Mgeni
rasmi katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne mwaka 2017
yaliyohudhuriwa na wazazi na wageni mbalimbali alikuwa mkuu wa wilaya ya
Shinyanga,Josephine Matiro.
Akizungumza
katika mahafali hayo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
alisema mabadiliko yoyote yanaletwa na ushirikiano hivyo kupitia
ushirikiano.lisema shule hiyo imekuwa maarufu nchini kutokana na elimu
bora inayotoa na kutokana na hali hiyo imeupatia sifa mkoa wa Shinyanga.
“Sisi
kama serikali tunajivunia uwepo wa shule hii katika mazingira yetu kwani
inatutangaza, tupo tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto
zinazojitokeza ili kusukuma gurudumu la maendeleo”,alieleza Matiro.“Tupo
tayari kuhakikisha kuwa tunashirikiana na sekta binafsi na milango yetu
ipo wazi na panapotokea changamoto msisite kutufikia”,alisema.
Alitumia
fursa hiyo kuwahamasisha wazazi kuwekeza kwenye elimu kwa watoto kwani
huo ndiyo urithi wenye thamani katika maisha yao.Katika hatua nyingine
aliipongeza shule hiyo kuajiri watu 63 katika shule kwani wanaunga mkono
lengo la serikali la kuzalisha ajira kwa wananchi.
Aidha
aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha shule ya awali na msingi
kitendo ambacho kinatokana na ushirikiano uliopo kati ya shule na
wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele kusukuma maendeleo ya shule.
Matiro
aliwataka wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kuwa mfano katika maeneo
wanakokwenda na kuhakikisha matendo yao yanaendana na mambo
waliyofundishwa shuleni.Naye Mkurugenzi wa shule ya Kom Sekondari
Jackton Koyi aliishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiwapa
katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inafikia malengo yake.
Alisema
Kom sekondari shule hiyo imetimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake na
imekuwa daraja la elimu kwa wanafunzi ambao wengi wamekuwa wakiingia
kidato cha tano na kujiunga katika vyuo mbalimbali.“Shule yetu imekuwa
ikifanya vizuri katika mitihani,mfano kati ya wanafunzi 160 waliomaliza
kidato cha nne mwaka 2015,145 walijiunga na masomo ya kidato cha tano,na
mwaka 2016 kati ya wanafunzi 144 waliofanya mtihani wa kidato cha
nne,133 walijiunga kidato cha tano”,aliongeza Koyi.
“Naomba
wazazi muendelee kutuamini na kuleta wanafunzi katika shule hii ambayo
imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali”,alieleza Koyi.Kwa
upande wake mkuu wa shule hiyo,Mwita Warioba alisema shule hiyo hivi
sasa ina jumla ya wanafunzi 542,walimu 32 huku akisisitiza kuwa lengo la
shule hiyo ni kutoa elimu bora na tayari shule hiyo pia imeanzisha
shule ya awali na msingi.“Shule yetu ina miundo mbinu ya
kutosha,madarasa yapo ya kutosha,tuna umeme wa Tanesco,maji kutoka ziwa
Victoria,mabweni 8,viwanja vya michezo,maktaba moja,maabara mbili
ikiwemo ya Computer”,aliongeza Waryoba.
Awali
akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne,Jackline Benson
alisema walianza kidato cha kwanza wakiwa 104,ambapo wavulana walikuwa
52 na wasichana 52 lakini idadi iliongezeka na hivyo idadi ya
waliohitimu kidato cha nne mwaka huu ni 154,kati yao wasichana ni 73 na
wavulana 81.
Wahitimu
wa kidato cha nne mwaka 2017 katika shule ya sekondari Kom wakimpokea
mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya shule hiyo,mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi
wa shule ya sekondari Kom,Jackton Koyi akimpokea mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro kwa ajili ya kushiriki mahafali ya kidato cha
nne katika shule hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwapungia mkono wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Kom .
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya mkurugenzi wa shule ya sekondari Kom .
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu Zena Ali akimweleza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro historia ya shule ya sekondari Kom wakati wa maonesho
ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika shule hiyo
Wanafunzi
wa shule ya sekondari Kom wakionesha ramani ya dunia kwa mkuu wa wilaya
ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa maonesho ya taaluma wakati wa
mahafali hayo
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu Rajuu Masudi ambaye ni mtaalamu wa kuchora akieleza
kuhusu sanaa ya uchoraji inayofanywa na wanafunzi wa shule ya sekondari
Kom
Mwanafunzi
wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kom,Safia Ali akitoa
maelezo kuhusu maonesho ya sayansi kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro
Wahitimu wa kidato cha nne 2017 katika shule ya sekondari Kom wakiandamana
Wahitimu wakiandamana kuelekea ukumbini
Mgeni
rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe wakati
wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari
Kom.Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule Peter Kugulu,kushoto ni
mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi
Wahitimu wakiingia ukumbini
Mkuu wa shule ya sekondari Kom,Mwita Waryoba akielezea historia ya shule hiyo
Mkurugenzi
wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi akizungumza wakati wa mahafali
ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom
Wahitimu wa kidato cha nne wakipunga mkono
Wahitimu wa kidato cha nne,Scholastica Simon na Dickson Nyansika wakikata keki wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka 2017
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimlisha keki mhitimu wa kidato cha nne Dickson Nyansika
Mahafali yanaendelea
Wanafunzi wakiwa wamevaa mavazi mbalimbali ya ubunifu
Wanafunzi wakiimba shairi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza 
Post a Comment