KADRI
siku zinavyokwenda mbele, wadau wanaoguswa na sanaa hapa nchini
wanasaka namna ya kusaidia tasnia hiyo ambayo ni eneo adhimu kwa jamii
duniani. Mara nyingi wasanii wamekuwa wakilalamika kwamba wanafanywa
kama yatima ambao wanakosa msaada wa kuwasogeza katika njia ya maendeleo
baada ya kufanya kazi zao kwa ufanisi. Wasanii hulalamika katika
matukio mbalimbali ya kazi zao, hali ambayo husababisha kuonekana kwamba
tasnia hiyo sio eneo la kukimbilia kwa sababu ya malalamiko kutoka kwa
baadhi ya wasanii.
Wasomi
wa Sanaa hapa nchini wanaguswa kwa kiasi kikubwa na sanaa za Tanzania
ambao wanatekeleza kwa vitendo kazi hizo, Asasi ya East Africa Art
Biennale (EASTAFAB) inaguswa na malalamiko, vilio vinavyotolewa na
baadhi ya wasanii katika matukio yanayoandaliwa na baadhi ya wadau
wanaoguswa na mdororo wa maendeleo ya kazi za sanaa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa EASTAFAB, Dr. Kiagho Kilonzo anasema mguso huo umejikita
kwenye kupromoti sanaa za Ufundi ambazo zina idadi kubwa ya wasanii
ambao wakiwemo Wachongaji, Wachoraji, Wasusi, Wafinyanzi na wengineo
ambao wanaingia kwenye Sanaa za Ufundi.
Dr.
Kilonzo anasema promosheni hiyo hufanyika kupitia Maonesho ya Sanaa
ambayo yalianza tangu mwaka 2003 ambayo hufanyika kila baada ya miaka
miwili. Anasema mara zote 7, maonesho hayo ya Afrika Mashariki yamekua
yakifanyika jijini Dar es Salaam ambayo pia hushirikisha wasanii wengine
kutoka nje ya Afrika Mashariki na kushirikisha wasanii wa Afrika, Ulaya
na Amerika lakini mwaka huu limepanua wigo kwa kufanyika katika majiji
ya Afrika Mashariki.
Anasema
pamoja na kufanyika katika majiji ya Afrika Mashariki pia kutakuwa na
semina ya wasanii na matukio mengi yanayoendana na mwenendo wa hali ya
sanaa pamoja na masoko ya sanaa.Dr. Kilonzo anasema katika semina hiyo
itakayofanyika Novemba 3, kutakuwa na wawasilishaji mada wa nchi za
Tanzania (kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania), Revocatus Kundy, Kenya
(kutoka Taasisi ya Elimu Kenya), Dr. Jennifer Wambugu na Uganda (kutoka
Kituo cha Maendeleo ya Mitaala), Christopher Muganga.

Katika
semina hiyo mbali ya watoa mada kuchanganua mipangilio mbalimbali ya
sanaa pia wasanii watajadili hoja mbalimbali zitakazowasilishwa mezani
na watoa mada. Dr. Kilonzo anasema pamoja nao katika semina hiyo
kutakuwa na wahusika wa masoko ya sanaa hapa nchini ambao ni pamoja na
Origenes Uiso (Karibu Art Gallery), Abel Shuma (Alliance Francaise), Tim
Amstrong kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Franciscar
Shirima-Frankoo Design.
Anasema
semina hiyo itafanyika nyumbani kwa Balozi wa Uswiss, Arthur Mattli
Masaki mtaa wa Kenyata Drive jijini Dar es Salaam ambaye pia atazindua
maonesho hayo Novemba 4 katika kituo cha Nafasi Art Mikocheni jijini Dar
es Salaam huku ufunguzi wa kwanza utafanyika Novemba 2 ambao utafanywa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa
Olle Gabriel.
Dk. Kilonzo anasema mgeni rasmi Novemba 3 atakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu, Habib Fent.
Dr.
Kilonzo anasema miaka 7, maonesho yalikuwa yakifanyika Nafasi Arts
Space, Alliance Francaise, Goeth Institut na Russian Culture
Centre.Aidha Dr. Kilonzo ambaye ni mhadhiri wa Sanaa wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM) anasema maonesho ya mwaka huu yataanza Novemba
2-22 ambayo yatashirikisha wasanii 100 wa sanaa za Ufundi.
Dr.
Kilonzo anasema kuanzia Novemba 28-Desemba 4, maonesho hayo
yatafanyika kwenye ukumbi wa Afrika Mashariki jijini Arusha ambako
wasanii wataonesha kazi zao katika ukumbi huo wa Kimataifa.
Anasema
baada ya maonesho ya jijini Arusha, yatahamia jijini Nairobi kuanzia
Januari 22-28 mwakani huku kuanzia Februari 2-8 yatafanyika jijini
Kampala wakati kuanzia Februari 12-18 yatafanyika jijini Kigali na
kumalizia jijini Bujumbura kuanzia Februari 22-28. Dr. Kilonzo anawataja
wafadhili waMaonyesho haya yamefadhiliwa na GIZ kupitia Asasi ya
Incubator for Integration for Development in East Africa (IIDEA) iliyopo
Arusha, pamoja na Balozi za Uswizi, Ujerumani, Denmark na Ubeligiji.
Wengine ni pamoja na vituo vya utamaduni wa kifaransa (Alliance
Francaises) vya Dar es Salaam, Nairobi na Kampala, Taasisi za kifaransa
(French Institutes) za Kigali na Bujumbura, kituo cha Nafasi Art Space
(Dar es Slaam), Kuona Art Trust (Nairobi), ghala za GoDown na Banana
Hill zilizoko Nairobi, pamoja ghala la AKA Gallery lililoko Kampala,
Goeth Institut, Swiss Airline na Dow ELEF International ya jijini Dar es
Salaam.
Dr.
Kilonzo anaweka bayana taratibu za ushiriki hufanyika kwa mtindo wa
kufanya matangazo kwa wasanii wa sanaa za Ufundi na Kamati ya maandalizi
ya maonesho hayo wanapitia majina na kuyapitisha majina 100 ya wasanii
watakaoshiriki.
Pamoja
na maonesho hayo kushirikisha wasanii wa Afrika Mashriki pia wamefungua
milango na nchi nyingine nje ya Afrika Mashariki ambazo zilishiriki
maonesho ya mwaka 2015 ni pamoja na Ghana, Ujerumani, Namibia, Burundi,
Msumbiji, Ufaransa, Ubelgiji na Marekani.
Mwaka huu nchi shiriki ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Norway, Ghana, Nigeria, Ubelgiji na India.
Anasema
pamoja na hayo wasanii washiriki wa maonesho hayo wanapata nafasi ya
kutangaza kazi zao katika jarida lao ambalo litasambazwa duniani kote.
“Kwa
mipangilio hiyo tutakuwa tumewasaidia kwa kiasi kikubwa wasanii wa
Sanaa za Ufundi ambao masoko yao yatafanyika moja kwa moja na wateja
katika nchi mbalimbali duniani, hivyo wasanii wajiandae kwa hilo,”
alisema Dr. Kilonzo.
Anaeleza
kwamba maonesho ya mwaka huu ni tofauti na maonesho yaliyopita kwani
mwaka huu wamefanikiwa kupata wadhamini ambao wamewasaidia kufanikisha
matukio yote muhimu, tofauti na mwaka 2015 walikuwa na matatizo ya fedha
ndio maana walifanya eneo moja la Afrika Mashariki ambalo ni Dar es
Salaam.
Dr.
Kilonzo anasema katika maeonesho hayo katika kila jiji kutakuwa na
makundi ya ngoma za asili yatakayosindikiza maonesho hayo ambayo
yatafanikisha kazi zao katika ufunguzi wa maonesho hayo.
Dr.
Kilonzo anaweka bayana uongozi unaounda taasisi ya EASTAFAB, ni pamoja
na waasisi Profesa Elias Jengo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi, Yves Goscinny Mratibu wa Mambo ya Nje, mratibu wa mipango
Stephen Ndibalema, Ofisa Habari na Mawasiliano, Boniphace Mkindi na
Francisca Shirima Mjumbe wa Bodi.



Post a Comment