Filbert
Rweyemamu,Arusha
Idadi ya vijana
wa Tanzania walioshiriki mashindano ya kubuni alama za mwonekano mpya wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) zikiwemo bendera na nembo imekua kubwa
ukilinganisha na washiriki wa nchi nyingine kwa pamoja.
Jumla ya kazi za
ubunifu 373 zilizowasilishwa kutoka nchi sita ambazo ni wananchama wa EAC
watanzania pekee walioshiriki kwa kutuma ubunifu wao ni 238.
Mratibu wa
Mawasiliano katika Sekretariati ya EAC,Florian Mutabazi ameliambia Mwananchi
kuwa waliotuma kwa njia ya barua pepe walikua 141 na posta 97 huku washiriki
saba wakishindwa kutambulisha utaifa wao.
Ametaja idadi ya
washiriki kutoka nchi nyingine kuwa Uganda ni 54, Kenya 40, Rwanda 19, Burundi
13 na mwanachama mpya wa EAC,Sudani Kusini ilipata washiriki wawili tu.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inakusudia
kupitia mashindano hayo kupata mwonekano mpya utakaokidhi matakwa ya sasa ya
idadi ya wanachama na kuwa na utambulisho ambao ni rahisi kwa mwananchi yeyote
kuutambua.
Pia EAC ina
taasisi kadhaa miongoni mwa hizo ni Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika
Mashariki(EAKC) yenye makao yake Zanzibar,Kamisheni ya Bonde la Ziwa
Victoria(LVBC) na nyingine ambazo zipo katika utaratibu maalumu wa kuwa na
utambulisho unaojiungamanisha na nembo ya EAC.
Mradi huu ukiacha
zawadi watakazopata washindi wa watatu wa mwanzo jumla ya dola 35,000 ambazo ni
zaidi ya Sh 77 milioni pia gharama nzima ya kuipatia EAC na taasisi zake utambulisho
mpya inafikia dola 200,000 sawa na
Sh 446 milioni.

Post a Comment