Wananchi
wa Wilayani ya Kwimba wamejitokeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa
wakati zoezi hilo likiendelea. Mpaka sasa idadi kubwa ya wananchi wa
Kwimba wameshasajiliwa huku mwitikio wa wananchi ukiongezeka na
kuonyesha ni kiu ya wananchi katika kupata Vitambulisho cha Taifa.
Afisa
Usajili Wilaya ya Kwimba Ndg Nelson Liyenge amewakumbusha wananchi
kujitokeza kwa wingi ili wasajiliwe kwa wakati na kuwawezesha kupata
Vitambulisho vya Taifa.
Umati
mkubwa wa Wananchi wa wilaya ya Kwimba wakisubiri kuingia kwenye chumba
ambacho Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unafanyika.
Wananchi
wa Wilaya ya Kwimba wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Msimamizi wa
Kituo cha Usajili juu ya mambo msingi wanayotakiwa kuzingatia pindi
watakapoingia kwenye chumba cha Usajili wakati wa kuchukiliwa alama za
kibaiolojia, picha na saini ya kielektroniki.
Wananchi mbalimbali Wilaya ya Kwimba wakiwa kwenye harakati za Usajili.
Mmoja wa wananchi wa Kwimba akiwa tayari kupigwa picha ikiwa ni sehemu ya hatua za usajili Vitambulisho vya Taifa.





إرسال تعليق