Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na
Viongozi na watumishi wengine wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini
(GPSA) Mkoa wa Kagera (hawapo pichani) alipotembelea ofisi hizo kuhusu
kuhakikisha Taasisi zote za Serikali zinapata huduma kutoka Wakala huo,
alipofanya ziara katika Mkoa huo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maagizo
kwa Kaimu Meneja wa Wakala Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa
Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi, kuhusu kuwahudumia Taasisi zote za
Serikali kwa kuwa ndio wajibu wa Wakala huo, alipofanya Ziara katika
Ofisi hizo za Mkoani Kagera.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawiro akielezea namna atakavyoshirikiana na Wakala wa
Ununuzi na Ugavi Serikalini katika Mkoa huo ili kuhakikisha kunakuwa na
matumizi adili ya fedha za Serikali, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea Ofisi za Wakala huo Mkoani Kagera.
Kaimu
Meneja wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera,
Bi. Dorothea Bugenyi (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) namna tetemeko la ardhi
lilivyo haribu miundombinu ya Ofisi hizo, alipotembelewa na Naibu Waziri
huyo katika Ofisi za GPSA Mkoani humo.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawiro (kulia) akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) alipotembelea Ghala la
Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoani Kagera.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili
kulia) akitembelea maeneo ya Ofisi za Wakala wa Ununuzi na Ugavi
Serikalini (GPSA) ambapo aliweza kupata maelezo namna Wakala huo
unavyofanya kazi.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa nne
kushoto), Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro (wa tano kulia), Kaimu Meneja wa Wakala wa
Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi
(wa tatu kushoto) na watumishi wengine wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kumalizika kwa ziara ya Naibu Waziri huyo katika Ofisi hizo
Mkoani Kagera.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, Kagera
NAIBU
waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameziagiza Mamlaka na
Taasisi zote za Umma kufanya ununuzi wa vifaa na mafuta kupitia Wakala
wa Serikali wa ununuzi na ugavi (GPSA) kwa mujibu wa sheria iliyotungwa
na Bunge na kuwaonya wahusika wote watakaoendelea kukaidi maagizo hayo
kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.
Dkt.
Kijaji ametoa maagizo hayo mkoani Kagera baada ya kutembelea na kukagua
shughuli zinazofanywa na Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoani humo na
kubaini kuwa taasii na idara nyingi za umma zinafanya manunuzi nje ya
mfumo wa GPSA jambo ambalo amesema ni ukiukwaji mkubwa wa sheria.
Alisema
kuwa lengo la Serikali la kuanzishwa kwa wakala huo pamoja na mambo
mengine ilikuwa kudhibiti matumizi ya Serikali na kuonya kuwa Serikali
haitakubali kuona sheria zinakiukwa kwa makusudi na kwa malengo
yanayoonesha kuna nia isiyo njema katika matumizi ya fedha za umma.
“Hili
si ombi ni maelekezo na ni agizo, taasisi zote zipate huduma kutoka kwa
wakala wetu (GPSA) kwani Serikali ilikuwa na dhamira ya uwepo wa
matumizi sahihi ya fedha za matumizi wanazopelekewa na ndiyo maana
ukaanzishwa Wakala huu” Alisema Dkt. Kijaji
Mkuu
wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro, akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa
mkoa wa Kagera, aliiagiza Wakala wa Ununuzi na Ugavi (GPSA) mkoani humo
kumpelekea orodha ya taasisi ambazo hazitumii huduma za wakala huo ili
aweze kuchukua hatua.
Alisema
kuwa ni jambo lisilofaa kwa Taasisi za Umma kukiuka sheria na kwamba
watatekeleza maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
haraka ili kuokoa fedha za Serikali na kuweka uwajibikaji.
Awali,
Kaimu Mkuu wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoa wa Kagera Bi.
Dorothea Bugenyi alieleza kuwa katika kipindi cha miaka 3 iliyopita
Wakala huo umeongeza makusanyo yatokanayo na mauzo ya vifaa na mafuta
kutoka Shilingi bilioni 1.9 hadi kufikia Shilingi bilioni 2.34.
Alisema
kuwa mapato hayo yangekuwa makubwa zaidi endapo taasisi zote za umma
zingetii sheria na kufanya manunuzi yao ya vifaa na mafuta kutoka kwa
Wakala huo na kuiomba Serikali kuusaidia Wakala huo kuziagiza taasisi
zake za umma kutekeleza sheria hiyo kwa vitendo.
No comments:
Post a Comment