Meneja Abdallah Mrisho na mkewe, Catherine Mdamu wakiwa katika pozi la furaha, muda mfupi baada ya kufungwa kwa ndoa yao.
Meneja Mrisho na mkewe, wakiwa na wanafamilia (walioshika magazeti), wakifurahi kwa pamoja baada ya kufungwa kwa ndoa yao.
Bibi
Harusi, Catherine (katikati) akiwa na wanafamilia (wenye nguo nyeupe)
na wafanyakazi wenzake, Women With Voices (WWV) wenye nguo za bluu.
Daaab! Maharusi na wanafamilia wakiwa katika pozi maarufu kwa jina la dab!
Maharusi wakiwa na wapambe wao, Said Mdoe na mkewe
Wakifurahia jambo baada ya kufungwa kwa ndoa yao.
Meneja
wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, jana (Jumamosi, Sept. 30,2017)
alifunga ndoa ya kifahari na Catherine Mdamu, iliyolifanya Jiji la Dar
es Salaam lisimame kwa muda, ikifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Katika sherehe hiyo, wafanyakazi wa Kampuni
ya Global Publishers wakiongozwa na mkurugenzi wao, Eric Shigongo, jamaa
na marafiki, walijumuika kula, kunywa mpaka kusaza na kucheza muziki
mzuri, mpaka usiku sana huku kukiwa na 'special appearance' ya Mbunge wa
Mtama, Nape Nnauye.
Harusi ya Abdallah na Catherine, Mlimani City - Part 1

إرسال تعليق